Mlezi wa familia ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na kiongozi wa ukoo wa Burito Nyerere, Chifu Japhet Wanzagi, amemkaribisha mgombea wa nafasi ya Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitis chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan, kutembelea ukoo wa Burito Nyerere na familia ya Baba wa Taifa huko Mwitongo, Butiama mkoani Mara.
Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwa Mwalimu Nyerere,Leo Oktoba Mosi mwaka 2025, Chifu Wanzagi amesema kuwa Dkt. Samia Suluhu Hassan atapokelewa kwa heshima kubwa kama kiongozi wa machifu hapa nchini, kwa kuzingatia mila na desturi za Wazanaki.
Kwa Mujibu wa Chifu Wanzagi Baada ya mapokezi hayo,Dkt Samia atatembelea nyumbani kwa Baba wa Taifa kwa ajili ya kuzuru kaburi na kuzungumza na wanafamilia, kabla ya kuanza Kampeni zake rasmi mkoani Mara kwa ajili ya kunadi sera za Chama Cha Mapinduzi.






