Chege Alia na Neno "Mamlaka"Linavyopandisha Gharama za Maisha Kwa Wananchi wa Shirati

GEORGE MARATO TV
0


MGOMBEA Ubunge wa jimbo la Rorya mkoani Mara Jafari Wambura Chage ameonesha kusikitishwa na kitendo cha wananchi wa Shirati jimboni humo kupandishiwa gharama za huduma kwa madai kuwa eneo hilo linastahili kuwa mji mdogo wakati mchakato wake haujakamika.

Chege ametoa kilio hicho mbele ya mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi ya chama cha mapinduzi Fadhili Maganya wakati akiomba kura kwa maelfu ya wananchi wa Michire eneo la Shirati.

Amesema wananchi hao wanekuwa katika mateso makubwa ya kupandishiwa huduma mbalimbali zikiwemo za nishati ya umeme,maji na viwanja kwa kutumia jina la "Mamlaka"huku wahusika wakijua wazi kuwa  mchakato huo haujakamilika.

 "Maji katika Mji wa Shirati na Vitongoji vyake haijakidhi huitaji wa huduma kwa Jamii.

*Lazima tupambanie hii,Gharama za Maisha Kwa jamii ya Shirati na Raranya,yamfanya kushtuka na Neno Mamlaka ya Mji"alisema Chege huku akishangikiwa na maelefu ya wananchi wa eneo hilo.

 "Amesema pamoja na Mamlaka hakuna,lakini uendeshaji wa Mahitaji ya Maisha Kama Umeme utumia rate ya Mamlaka, Vijijini Mwananchi anavuta Umeme kwa kuchangia Tshs 27,000 hapa Shirati kuvuta Umeme kwa shilingi 300,000,Uvutaji wa Maji Nyumbani gharama nazo zipo juu tofauti na maeneo mengine,Kisa Mamlaka yasiyokuepo"alisema

Kwa sababu hiyi amemwomba mgeni rasmi katika mkutano huo wa kampeni Mwenyekiti wa Wazazi Taifa  Abduli Fadhili Maganya  kusaidia utatuzi wa jambo hilo hasa kwa Kupatikana ukamilifu wa Mamlaka ya mji na Kama hakuna uwezekano kwa sasa Neno hilo lifutwe ili  kuwapunguzia wananchi gharama za Maisha

Katika mkutano huo Chege ameomba wananchi kujitokeza  kumpigia kura nyingi mgombea wa nafasi ya Urais kupitia CCM dkt Samia Suluhu Hassan,yeye mwenyewe ili awe mbunge wa kipindi kingine cha pili wakiwemo madiwani wanatokana na CCM.

Uchaguzi mkuu wa Rais,wambunge na Madiwani unatarajiwa kufanyika Oktoba 29 mwaka huu wa 2025.








Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top