Na Angela Sebastian;Bukoba
Serikali ya hawamu ya sita imewaondolea adha ya kutembea kilometa 15 wanafunzi wa kata ya Katerero iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba kwenda kusoma katika shule ya sekondari ya Bujunangoma iliyopo kata jirani ya Kemondo.
Hiyo imetokana na kuwajengea shule ya sekondari inayotoa mafunzo ya amali iliyogharimu shilingi bilioni 584 ambayo imezinduliwa leo na mbio za mwenge wa uhuru Kitaifa 2025.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ismail Ali Ussi amewataka vijana hususani wanafunzi kuchangamkia fursa hiyo ya Elimu ambayo itawezesha kujiajiri pindi watakapo hitimu masomo yao.
Ussi amesema kuwa lengo la Serikali ya hawamu ya sita ni kujenga shule hizo zenye mchepuo wa amali, ni kuwezesha vijana kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira pindi wanapohitimu masomo yao.
Aidha emewashauri wananchi wa Halmashauri ya Bukoba kujitokeza kwa wingi kupiga kura ifikapo Oktoba 29 mwaka huu ili kuwachagua viongozi watakaowaletea maendeleo ya kweli.
Akitoa taarifa kwa kiongozi wa mbio za mwenge,mkuu.wa shule hiyo Ferdinand Eladius amesema shule hiyo imekuwa msaada kwa wanafunzi wa kata Katerero ambao walikuwa wakitembea umbali wa kilometa 15 kufuata elimu katika shule ya Bujunangoma iliyoko kata jirani ya Kemondo.
Pia wanafunzi wa shule hiyo wamepongeza juhudi za Serikali kwa kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu na kushindwa kuhudhulia masomo kwa wakati ambapo wamesema masomo ya amali yanatawezesha kupata ujuzi mbalimbali wa kiufundi na kubaini vipaji vyao.
Irine Ptojestus na Aidan Johansen ni wanafunzi wa shule hiyo wanasema walikuwa wakiamka saa kumi na moja alfajiri ili kuanza safari ya kwenda katika shule ya jirani ya Bujunangoma ambayo ipo kata jirani ya Kemondo hari iliyosababisha kusinzia ovyo darasani na usalama wao ulikuwa mashakani.
Pia mwenge wa uhuru umeweka jiwe la msingi barabara ya Kyetema-Katerero yenye urefu wa Kilometa 0.55 ambayo itagharimu kiasi cha zaidi ya shl miln 253.
Wakati akipokea mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Bukoba kutokea wilaya ya Muleba,,mkuu wa wilaya ya Bukoba Erasto Sima amesema kuwa mwenge huo ukiwa katika Wilaya ya hiyo utatembea kilometa 81.5. na kukagua,kuweka mawe ya msingi na kuzindua Miradi 14 yenye thamani ya shilingi bilioni 8.8.