Na Angela Sebastian Kagera
Katibu wa siasa,uenezi na mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kagera Amim Mohamud amesema, mgombea mwenza wa Urais,Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi anatarajiwa kuwasili mkoani Kagera Septemba sita mwaka huu kwa ajili ya kunadi sera,Ilani ya CCM 2025-2030 na kuomba kura.
Mahmud amesema Dkt.Nchimbi atapokelewa Wilayani Biharamulo Septemba sita atahutubia wananchi katika eneo la Nyakanazi ambapo Septemba saba atafanya mikutano ya adhara katika Wilaya za Ngara,Kyerwa,Bukoba vijijini na mjini ambapo atahitimisha ziara yake.

