Doyo kuzindua kampeni za Urais Tanga

GEORGE MARATO TV
0


Na Mwandishi Wetu, Tanga

MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha National League for Democracy (NLD), Doyo Hassan Doyo, Septemba 4, 2025 atazindua kampeni zake za kugombea Urais katika viwanja vya Komesho Jijini Tanga.

Katibu wa Chama hicho mkoani Tanga Boniface Gidion alisema maandalizi ya mkutano huo yamekamilika na viongozi wa Chama hicho ngazi ya kitaifa wakiongozwa na Mwenyekiti Mfaume Hamisi Hassan tayari wapo Jijini Tanga kwa ajili ya uzinduzi huo.

Alisema Doyo ambaye licha ya kugombea Urais, pia ni Katibu Mkuu wa Chama hicho, ameongozana na mgombea mwenza, Chausiku Khatibu Mohamed.

Katika hatua nyingine mgombea huyo wa Urais kupitia Chama hicho, amepokelewa kwa heshima ya kipekee na kufanyiwa dua maalum na wazee wa Kijiji cha Misima, Wilaya ya Handeni, mkoani Tanga.

Wazee wa kijiji hicho walijitokeza kwa wingi kumpokea Mhe. Doyo na kumfanyia dua za kumtakia kheri, baraka, na mafanikio katika safari yake ya kisiasa ya kuwania nafasi ya juu kabisa ya uongozi wa Taifa.

Akizungumza kwa niaba ya wazee wa Misima, mmoja wa viongozi wa kidini Abdallah Samlimbo alisema, “Misima ni sehemu yenye historia kubwa ya mapambano ya ukombozi wa Taifa hili.

"Tunamwona Mhe. Doyo kama kijana aliyepita katika nyayo zile zile za wazee wake waliopigania uhuru. Uthubutu wake ni wa kipekee na utakumbukwa na vizazi vijavyo hapa Misima.”

Kwa upande wake, Mhe. Doyo aliwashukuru wazee hao kwa mapokezi yao yenye heshima na maombi yao ya baraka.






Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top