RAIS EVARISTE NA WAZIRI MKUU WA TANZANIA WAZINDUA UJENZI WA RELI YA KISASA NCHINI BURUNDI.

GEORGE MARATO TV
0

 

Rais wa Jamhuri ya Burundi Evariste Ndayishimiye akiwa na waziri mkuu wa Tanzania wamefanya uzinduzi rasmi wa ujenzi wa  reli ya kisasa (SGR) katika wilaya ya Musongati mkoani Burunga nchini Burundi.


Katika shughuli hizo Rais wa Burundi aliweka jiwe la msingi pamoja na waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa eneo la ujenzi kuashiria kuanza kazi rasmi za ujenzi wa reli.

Waziri wa madini na maliasili wa Tanzania anayeongoza ujenzi wa reli hiyo, Makame Malawa kwanza amesema kuwa reli hiyo itasaidia kupunguza gharama za usafirishaji wa bidhaa hadi 70%.


Rais Evariste Ndayishimiye amempongeza Rais wa Tanzania mhe.Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake ili zoezi hilo liweze kufanikiwa ambapo reli hiyo iraendelea kujenga uhusiano katika ya nchi mbili kupitia sekta mbali mbali ikiwemo ya madini.

Waziri mkuu wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa amesema uzinduzi wa ujenzi wa reli hiyo ni historia kwa nchi hizo mbili katika uhusiano kati ya Warundi na Watanzania.

Burundi na Tanzania zimekuwa na uhusiano si katika biashara tu bali hata katika mambo ya demokrasia kwani Tanzania ilikuwa na mchango kubwa ili Burundi ipate uhuru wake.




Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top