Akiwa na umri wa miaka 80, Rais Yoweri Museveni amepuuza wito wa kustaafu, huku wakosoaji wake wakimshutumu kwa kuanza njia ya kimabavu bila upinzani wowote, hata ndani ya chama chake tawala cha National Resistance Movement (NRM). Museveni alichukua madaraka kwa mara ya kwanza kama Kiongozi wa kikosi cha waasi mwaka 1986.
Tangu wakati huo amechaguliwa mara sita, ingawa chaguzi za hivi karibuni zilikumbwa na ghasia na madai ya udanganyifu katika uchaguzi na Ukandamizaji wa Upinzani.
Mpinzani wake mkuu katika uchaguzi uliopita alikuwa msanii maarufu anayejulikana kwa jina la Bobi Wine, ambaye pia alitangaza kugombea katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Januari 2026.
Wine, ambaye jina lake halisi ni Kyagulanyi Ssentamu, ameona washirika wake wengi wakifungwa au kulazimishwa kujificha wakati vikosi vya usalama vilipopambana na wafuasi wa upinzani.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni, 80, amethibitisha nia yake ya kugombea katika uchaguzi wa Rais Januari mwakani licha ya kutawala nchi hiyo ya Afrika Mashariki tangu 1986.









Comments
Post a Comment