Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imesema itaendelea kuratibu na kusimamia masuala ya ajira nchi ili kutoa fursa kwa vijana kwa kuzingatia sera na maono ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Ridhiwan Kikwete alisema hayo wakati akiongoza na kuzindua Maonesho ya nne ya ajira kati ya Tanzania na China.
"Nawahakikishia Watanzania kuwa serikali kupitia wizara itaendelea kuratibu kwa tija masuala ya ajira nchini na kusimamia maslahi ya kisheria, sera na miongozo ya ajira na kazi na maono ya Rais," alisema Kikwete.
Maonesho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam yalikuwa na lengo la kutangaza na kuwaunganisha vijana wahitimu na wenye ujuzi na kuwaunganisha na makampuni ya Kichina.
Kikwete aliwakumbusha washiriki wa maonesho hayo umuhimu wa kuenzi ushirikiano ulioasisiwa na waasisi wa nchi mbili hizo lakini hatua mbalimbali zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kutatua changamoto ya ajira nchini.
Mhe Waziri alisema maonesho hayo ambayo yanatarajia kutoa fursa za ajira za moja kwa moja zaidi ya 2000.
"Maonesho haya ni kati ya hatua za serikali ya awamu ya sita katika kutatua changamoto za ajira nchini, kupitia maonesho haya makampuni ya China yanayofanya kazi hapa nchini yanaonesha mahitaji ya ujuzi wanaouhitaji ili vijana wetu waweze kuchangamkia fursa hizo na ni vema mkalinda uhusiano huu kwa ajili ya kudumisha kwa maslahi makubwa ya kupata ajira," alisema mhe Kikwete.
Aliwaomba vijana wenye sifa za mahitaji ya mahitaji ya makampuni hayo ya China kufuatia makubaliano yaliiwekwa baina ya nchi hizo, kujitokeza na kufanya kazi kwa weledi ili kuipa sifa nchi katika mahusiano hayo.
"Hivyo vijana wenye sifa za mahitaji ya makampuni ya hayo kufuatia makubaliano baina ya serikali zetu katika kufikia maendeleo endelevu ambayo nchi yetu itafaidika katika shughuli zinazofanywa na makampuni hayo nchi na kutoa fursa kwa vijana wetu wazawa wenye sifa wanazohitaji ni vema mkafanya kazi kwa weledi na sifa njema," alisema Kikwete.





Comments
Post a Comment