TARIME
KADA wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) Nicholas Mgaya Chichake amechukua fomu kuwania ubunge wa jimbo la Tarime Vijijini.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kuchukua fumu hiyo kwenye ofisi za chama hicho amesema kutokana na fursa zilizopo kwenye jimbo hilo wananchi hawapaswi kuwa na hali hizo za kiuchumi
Amesema serikali ya Dkt.Samia Suluhu Hassan mambo mengi ya maendeleo yamefanyika lakini bado wananchi hali zao za kimaisha hazijalisha.
Tunazo fursa za mgodi wa Barrick,Hifadhi ya Serengeti na ardhi ya kutosha lakini wananchi wetu hawako sawa mfukoni
" Ndugu zangu leo nimejitokeza kuchukua fumu jimbo la Tarime Vijijini ili nipiganie keki hii tuweze Ä·uila pamamoja.
" Ninao uwezo mzuri wa kuwapigania wananchi wa jimbo la Tarime Vijijini muda wa kula ukifika naomba wanichague kwa kula za kishindo",amesema Amesema.




Comments
Post a Comment