Mbunge wa Jimbo la Chalinze na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete Jana Juni 21, 2025 amepokea hundi yenye thamani ya milioni 52 kutoka Kiwanda cha KEDA kilichopo Chalinze mkoani Pwani kwa ajili ya kwenda kusaidia ukarabati wa Shule ya Msingi ya Chalinze iliyopo Jimboni kwake Chalinze.
Makabidhiano hayo yamefanyika Jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Johari Rotana ambapo hundi iliyotolewa ni sehemu ya mchango wa boksi 1,000 za tails ambapo vifaa hivi vitatumika katika ujenzi na ukarabati wa madarasa sita pamoja na kukamilisha bweni la wavulana wenye mahitaji maalumu.
Aidha, Kikwete amepokea vifaa vingine kutoka Kiwanda cha KEDA ambavyo ni kompyuta 20 na meza zake, televisheni yenye ukubwa wa inchi 43, mashine ya kutolea nakala (photocopy), kamera, mipira ya michezo pamoja na jezi za wachezaji.
Kikwete ameushukuru uongozi wa Kiwanda hicho na kutoa wito kwa wadau wengine kujitokeza katika kuchangia ukarabati wa shule hiyo ikiwa ni harakati za kuunga mkono juhudi za Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha sekta ya elimu.
Ikiwa ni kuelekea Maadhimisho ya miaka 67 tangu kuanzishwa kwa shule hiyo mnamo mwaka 1958 ambapo moja ya mikakati iliyowekwa na shule hiyo ni kukusanya jumla ya kiasi cha milioni 300 kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa miundombinu yake.






Comments
Post a Comment