Ruto:Siwezi Kuachia Mamlaka Kiongozi Yeyote aliye Upinzani Kwa Sasa

GEORGE MARATO TV
0

RAIS wa Kenya Dokta William Ruto ameapa kutokabidhi mamlaka kwa kiongozi yeyote aliye upinzani kwa sasa akisema wote wamechanganyikiwa na hawana ajenga kwa nchi.

Rais Ruto amesema Upinzani wanatafuta kitu kimoja tu, yaani kumwondoa mamlakani bila mipango yoyote mahsusi kwa manufaa ya Wakenya na maendeleo kwa nchi.

“Nimeona ajenda yao kuu ni ‘Ruto must go’. Hakuna kingine. Sasa, ‘Ruto must go’ itasaidiaje Wakenya wanaokumbwa na changamoto za matibabu, elimu na matatizo mengine?” alihoji Rais Ruto alipohudhuria ibada ya kanisa katika Shule ya Kivaywa eneo bunge la Lugari, Kaunti ya Kakamega. 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top