Misa Tan na Ewura yawajengea Uwezo Waandishi wa Habari Kuifahamu Ewura na Majukumu Yake

GEORGE MARATO TV
0


Mwandishi wetu ;Dar es salaam

Semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) pamoja na majukumu yake inaendelea leo katika ukumbi wa mikutano wa Beachcomber Hotel, jijini Dar es Salaam.

Semina hiyo imefunguliwa rasmi na Nyirabu Musira kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa EWURA, ambapo amesisitiza umuhimu wa waandishi wa habari kuelewa kazi na majukumu ya EWURA ili waweze kuhabarisha jamii kwa usahihi na ufasaha.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN), Edwin Soko ameishukuru EWURA kwa hiyo  hiyo, akisema kuwa ni hatua muhimu katika kuimarisha ushirikiano baina ya mamlaka hiyo na vyombo vya habari nchini.

Baadhi ya washiriki wa semina hiyo ambao ni wanachama wa MISA-TAN kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo Mwanza, Arusha, Pwani, Dar es Salaam na Shinyanga, wameahidi kuzingatia yale wanayojifunza kupitia mawasilisho mbalimbali na kwenda kuyatekeleza kwa vitendo katika kazi zao za kila siku za uandishi wa habari. 

Semina hiyo inaendelea, ikilenga kuimarisha uelewa wa wanahabari juu ya mfumo wa udhibiti wa sekta ya nishati na maji nchini.







Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top