Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa ametanga kuwa Mabaraza yote ya Halmashauri yanapaswa kuvunjwa ifikapo Tarehe 20/06/2025.
Ukomo wa Kamati zote za Halmashauri zinazoundwa na Madiwani utakuwa ni Tarehe 20/06/2025.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri husika atakuwa ndiye Mwenyekiti wa mpito wa Halmashauri akisaidiwa na Wakuu wa Idara kama sehemu ya Kamati hadi hapo Uchaguzi utakapofanyika.
Kwa taarifa hii hakuna Diwani atakayeendelea na majukumu yake mara baada ya Tarehe 20/06/2026!