Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

MwanaFA: Sasa nitalala usingizi baada ya kupatikana kituo cha afya tarafa ya Amani

📌 Zabuni ya ujenzi wa kituo hicho kutangazwa Jumatatu


Na Mwandishi Wetu, Muheza 


NAIBU Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Hamisi Mwinjuma maarufu MwanaFA, amesema kukosekana kwa kituo cha afya tarafa ya Amani kulikuwa kukimkosesha usingizi kwa kuwa hakutaka miaka yake mitano ya awali ya ubunge asimalize bila kupatikana kituo hicho.

Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi kiasi cha shilingi milioni 645.2 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa kituo hicho iliyofanyika katika eneo litakalojengwa  kwenye zahanati ya Kijiji cha Mgambo Miembeni, alisema suala la kituo lilitolewa ahadi na wabunge waliopita tangu mwaka 1998.

Alisema kituo hicho kilikuwa na siasa kubwa kutoka kwa watangulizi wake wa nafasi hiyo, hivyo kupatikana kwa kituo hicho ni faraja kwake na Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya wabunge waliopita kutoa ahadi bila mafanikio.

"Nimewahi kuja Amani mara nyingi sana lakini leo, nimekuja kama kidume kweli kweli, mara hii nimekuja Kifua mbele kama nimepigwa ngumi ya mgongo," alisema na kuongeza,

"Nalisema hili kwasababu sisi wengine tuna sifa nyingi lakini sifa ya uongo sina, miongoni mwa mambo yaliyokuwa yakinilaza macho, yaliyokuwa yakinikosesha raha na miongoni mwa mambo yaliyokuwa yakitumika vibaya kisiasa ni hili la kituo cha afya tarafa ya Amani,".

Alisema anamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kusikiliza maombi ya muda mrefu ya ujenzi wa kituo hicho yaliyowekwa na wabunge waliopita, hatimaye yeye amekwenda kutimiza ndoto za wananchi wa tarafa hiyo baada ya serikali kutoa fedha za ujenzi wake.

Alisema hoja ya kupata kituo cha afya tarafa ya Amani ilikuwepo tangu mwaka 1998 iliyoahidiwa na Julius Semwaiko aliyekuwa mbunge katika kipindi hicho na walipita wabunge wawili walishindwa na Sasa baada ya miaka 27, amefanikisha hilo.

Alisema mwaka 2023 aliwaeleza wananchi wa tarafa hiyo kwamba hadi ifikapo Juni mwaka huu endapo serikali isingetoa fedha hizo, angeanza ujenzi huo kwa kutoa shilingi milioni 100 ili wananchi waanze tofauti na aliyetoa matofari 500 kutaka kujengwa kituo hicho jambo ambalo alisema halikuwa sahihi na utani wa kisiasa.

"Subira mliokuwa nayo muda mrefu imezaa heri baada ya serikali kutoa fedha za mkupuo mmoja sh. 645,282,284 tofauti na maeneo mengine ambayo serikali inatoa fedha za kuanzia shilingi milioni 250," alisema MwanaFA.

Alisema dhamira yake ilikuwa ya dhati kabisa kuhakikisha kituo hicho kinajengwa kumaliza ndoto ya wananchi katika miaka yake ya kwanza ya ubunge katika Jimbo hilo ili wananchi waondokane na tatizo  la kufuata huduma za Afya mbali na tarafa hiyo.

Mbunge huyo alidokeza kwamba serikali pia imetoa shilingi milioni 250 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa kituo kingine cha afya katika tarafa ya Ngomeni ambacho kitajengwa kata ya Misozwe ili kukamilisha tarafa zote nne za wilaya hiyo kupata vituo vya afya. 

Tarafa nyingine ni ya Bwembera iliyokuwa na kituo cha afya kilichojengwa kata ya Kwafungo, tarafa ya Muheza iliyokuwa na vituo vya afya viwili kata ya Mkuzi na Mbaramo.

Akizungumzia kuhusu barabara MwanaFA ambaye wananchi wilayani hapa wanampenda kutokana na kuleta miradi mingi, alisema kuwa awali barabara ya Muheza-Amani yenye urefu wa kilomita 32 ilikuwa imewekwa lami kilomita 4 tu.

Lakini Sasa kwa miaka minne hii tayari MwanaFA amefanikisha barabara hiyo kufikia kilomita 13 kwa kiwango cha lami.

"Ndugu zangu mlinisikia Rais Dkt Samia Suluhu Hassan alipokuja Muheza nikimuomba kuhusu barabara hii na serikali katika mwaka huu wa fedha imenipa tena fedha za kujenga kilomita 4," alisema na kuongeza,

"Najua barabara hii bado inachangamoto kwa baadhi ya sehemu lakini mnaona wakandarasi wapo kazini wanajenga sehemu korofi kwa kuweka zege ili ipitie lakini niwaahidi nitaimaliza,".

Aliwataka wananchi wa tarafa hiyo kushirikiana na mafundi watakaojenga kituo hicho cha afya na wawe walinzi wa vifaa kuzuia watu wasiibe ili jengo hilo likamilike kwa wakati na kwa thamani ya fedha zilizotolewa.

Awali mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza Dkt Fani Mussa alisema kituo hicho ambacho zabuni yake itatangazwa Juni 16 mwaka huu, kitahudumia wakazi 39,792 kutoka kata sita za Kisiwani, Amani, Mbomole, Kwezitu, Zirai na Misalai.

Dkt Fani alimshukuru mbunge huyo katika kipindi chake kufanikisha idara ya afya kupokea kiasi cha sh. 6,542,584,369.6 ambazo zimetumika kwa kujenga miundombinu, ununuzi wa magari, madawa na vifaa tiba.

Katibu wa CCM wilaya ya Muheza Simon Leng'ese alisema kuwa chama hicho kimefurahishwa na kazi nzuri iliyofanywa na serikali kutoa fedha hizo ambazo zimeweza kutekeleza ilani ya Chama hicho kwa vitendo na kwamba kituo hicho kitaipa heshima serikali pamoja na chama kwa kuwa kimesubiriwa kwa muda mrefu.

"Huu mradi ulishindikana muda mrefu Sasa MwanaFA ameweza, Mama Samia hoyeee, mbunge hoyeee," alisema Leng'ese ambaye aliwataka wananchi wawaunge mkono viongozi wanaotatua changamoto zao.

Katibu wa Uenezi na siasa wa wilaya ya Muheza Mwedi Sufiani alisema wakati umefika kwa wananchi wa Muheza kuchagua watu wenye maarifa ya kutatua changamoto zao kamwe wasichague watu  wanaowapa fedha wakati wa chaguzi.

 "Tunataka viongozi wenye akili wanaoleta maendeleo kwa watu wake, siyo mtu anayetumia fedha lakini akashindwa kuleta maendeleo," alisema Mwedi.

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wilayani Muheza (UVCCM) Aziza Mshakangoto alimshukuru mbunge huyo kwa kufanikisha kituo cha afya na akawataka watu wanaotumia kituo cha afya kama mtaji wao kisiasa watafute kiki nyingine.

Aliwataka wananchi wa tarafa ya Amani wasiyumbe katika kuchagua wagombea ubunge na udiwani watazame watu walioleta maendeleo kikiwemo kituo hicho na waachane na watu wanaopitapita na kutoa sukari kwa watu wachache.

Diwani wa kata ya Misalai Said Mtunguja alimsifu mbunge kwa kusema kwamba katika kipindi chake amerahisisha kazi ya Siasa kwa kuwezesha wilaya hiyo kupata miradi mingi ya maendeleo katika kata zote za tarafa hiyo.

Alisema kuwa awali walianza ujenzi wa kituo hicho mwaka 2017 kwa kutumia michango ya wananchi lakini baada ya kuingia mbunge huyo alifuta michango hiyo na wananchi waliofunguliwa kesi kwa kutotoa michango kesi zao zilifutwa.

Hivyo, diwani huyo aliyesoma mistari mbalimbali ya biblia alisema kuwa Wagaratia sura 6 mstari 4 inasema "Kila mtu apimwe kwa kazi yake na ndipo azungumzie kazi ya mwenzake,".

Pia alinukuu kifungu cha biblia kutoa Mwanzo sura 43 mstari wa 45 kuwa "Chagueni mtu mwenye akili aweze kusimamia njaa ya watu kwa miaka Saba", alisema na kuongeza MwanaFA anaweza kusimamia njaa ya miaka Saba mara mbili.

Wananchi Mariamu Mtunguja na Said Baghaa waliahidi kumuunga mkono MwanaFA kutokana na kazi nzuri ambazo amezifanya katika tarafa hiyo ikiwemo kumaliza ndoto yao ya muda mrefu ya kupata kituo hicho cha afya.




Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

Wananchi Serengeti Wamtaja Dkt Rhimo Nyansaho Kama Chachu ya Maendeleo Kwao

Na Shomari Binda-GMTV  WANANCHI Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamemtaja Dkt.Rhimo Nyansaho kama chachu ya maendeleo kupitia taasisi yake ya Nyansaho Foundation. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na GMTV wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu mchango wake umeonekana katika kuisaidia jamii. Wamesema ukifika Jimbo la Serengeti kila Kata na Kijiji huwezi kukosa mkono wa Dkt.Nyansaho kuchangia na kusaidia jamii kuanzia elimu,afya,maji na masuala mengine ya jamii. Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mwita Sagati amesema wapo watu wanaojitokeza kusaidia jamii kipindi cha uchaguzi kwa kulenga kupata uongozi lakini imekuwa tofauti kwa Dkt.Nyansaho. Sagati amesema iwapo atajitokeza kuomba nafasi ya ubunge wapo tayari kumpambania na kumchagua ili aweze kuendelea kutoa mchango wake katika kusaidia jamii. " Tunashukuru sana mchango wa Dkt.Nyansaho kwa kuchangia shughuli za maendeleo hapa Serengeti. " Wengine huwa wanakuja nyakati za uchaguzi lakini huyu mchango wake ni ...

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...