Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni mjumbe wa halmashauri kuu ya Taifa ya chama cha Mapinduzi CCM mh Angelina Mabula,ameshiriki katika Mkutano Mkuu wa CCM Kata ya Bugogwa kwaajili ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa CCM katika Kata ya Bugogwa Kwa kipindi Cha 2020/2025.
Mkutano wakati wa Mkutano huo ambao Mhe Mabula alikuwa Mgeni rasmi amewapongeza viongozi wa Kata hiyo kwa kutekekeza kwa vitendo ilani ya CCM hukusimamia miradi ya maendeleo iliyoelekezwa na serikali katika kata hiyo.
" Naomba niwaongezee sanaa Wana CCM wa Kata ya Bugogwa kwani utekelezaji wa Ilani hii ambayo leo tunaipokea hapa kutoka kwa Mhe Diwani umetokana na kujenga Mkubwa na muunganiko uliopo baina ya wenyeviti wa serikali za mitaa ,Mhe Diwani , Mimi mwenyewe pamoja kama Mbunge pamoja na Mhe Rais wetu Dk Samia Suluhu Hassan.
Pamoja na hayo Mhe Mbunge alitumia nafasi hiyo kuwashukuru sana wa Kata ya Bugogwa Kwa kuendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi kwani huu ndio umepelekea utekelezaji wa miradi mbalimbali ndani ya Kata ya Bugogwa .
Naye Diwani wa Kata ya Bugogwa ndugu William Mashamba alitumia nafasi hiyo kuwashukuru sana Wana CCM wote Kata ya Bugogwa kwa wananchi walioutoa kwani umewezesha ufanikishaji wa miradi ya Maendeleo Ndani ya Kata hii.
Amempongeza pia mbunge wa jimbo hilo mh Mabula kwa kazi kubwa ya Maendeleo aliyoifanya katika kipindi hicho kwa kipindi hicho.