Na Shomari Binda-Musoma
MBUNGE wa Jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo amesema kongamano la maonyesho ya madini ya siku 4 mkoani Mara yameuchangamsha mji wa Musoma.
Licha ya kuuchangamsha mji yamewawezesha wajasiliamali kufanya biashara na kuwaongezea kipato na kuendelea na maisha.
Hayo yamesemwa na mbunge huyo wakati akitoa salamu kwenye kilele cha maonyesho hayo kilichofanyika leo juni 6,2025 kwenye uwanja wa shule ya msingi Mukendo.
Amesema ofisi ya mkuu wa mkoa kupitia sekta ya madini imefanya jambo kubwa ambalo limefikisha ujumbe namna sekta hiyo ya madini inavyoupaisha mkoa wa Mara na mji wa Musoma
Mathayo amesema kama wabunge wamepitisha bajeti kubwa na nzuri kwa Wizara ya Madini kwa kutambua mchango wake katika kuinua uchumi ukiwemo wa vijana.
Mbunge huyo amesema ametoka bungeni kuja kushiriki tukio hilo kwa kuwa linafanyika kwa wananchi anaowawakilisha bungeni na ni muhimu kujumuika nao.
" Nishukuru sana ofisi ya mkuu wa mkoa na Wizara ya Madini kwa maonyesho haya mazuri ambayo yameuchangamsha mji wetu wa Musoma na kuwafanya wajasiliamali kunufaika kiuchumi.
" Hapa Musoma tunao wafanyabiashara wa madini na wachenjuaji ambao kwa pamoja na kushirikiana na wachimbaji wanakwenda kuinua mji wetu na mkoa wa Mara kiujumla",amesema.
Akizungumza wakati akifunga maonyesho hayo Waziri wa Madini Antony Mavunde amesema mkoa wa Mara unakuja juu katika sekta ya madini kwa kusaidia pato la mkoa na taifa kwa ujumla.
Amesema serikali ya awamu ya 6 chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan inakuja na neema kubwa kwa wachimbaji kwa kuhakikisha kupitia sekta hiyo wanainuka kiuchumi.
Waziri Mavunde amesema ili kuona mambo mazuri yanaendelea kufanikiwa katika mambo 16 ya kuboresha sekta ya madini ni pamoja na kuanzisha vituo vya ukodishaji mitambo na wachimbaji wadogo kuchimbiwa kwenye maeneo yao.
Awali mkuu wa mkoa wa Mara kama mlezi wa wachimbaji wadogo mkoa wa Mara amesema wataendelea kuwasimamia vizuri wachimbaji wadogo na kuhakikisha wanakua
Amesema sekta ya madini inachangia pato la mkoa kwa asilimia 18 na kwa namna mambo yanavyokwenda vizuri wataendelea kuchangia zaidi.
Mapema asubuhi wachimbaji wadogo na wadsu wa madini walifanya matembezi ysliyoanzia ofisi ya mkuu wa mkoa hadi viwanja vya shule ya msingi Mukendo kumpongeza na kumshukuru Rsis Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa namna alivyosaidia kukuza sekta madini nchini.
Maonyesho hayo ambayo yamefanyika kwa mara ya kwanza mkoani Mara yameonekana kuwa na mafanikio makubwa.






