-Kigwangala Atoa Ushauri Ili "Derby" Ya Kariakoo Ichezeke Juni 15 Yanga Na Simba
Na Shomari Binda-GMTV
WAZIRI wa zamani wa Maliasili na mdau wa michezo Hamis Kingwangala ametoa ushauri ili mchezo huo. Uweze kuchezeka kama ulivyopangwa juni 15.
Moja ya eneo la ushauri wake alioutoa ni kumalizwa kwa mgogoro wa Yanga na Shirikisho la Mpira wa Miguu hapa Nchini( TFF).
Amesema mgogoro kati ya Yanga na TFF imefikia kiwango cha hatari anbapo Yanga wametangaza kutocheza mechi hiyo wakidai kunyanyaswa na TFF na Simba wanajipanga kushiriki.
Kigwangala amesema Ikitokea TFF wakampa Simba ushindi wa mezani Simba akawa bingwa halafu Yanga wakaadhibiwa taifa litaingia kwenye sintofahamu kubwa na Inaweza kusababisha vurugu za mashabiki, maandamano, migomo, au hata usalama wa raia kutishiwa.
Amesema serikali inaweza kukaa na pande zote na kuwa na mazungumzo ya kina na kufikia muafaka ili kuweza kuendeleza mchezo wa mpira wa miguu.
"Tulipofikia, mgogoro wa Yanga, Simba, TFF na Bodi ya Ligi siyo wa kupuuza haswa kwa kuzingatia huu ni mwaka wa uchaguzi ni lazima serikali iingilie kati kuleta usuluhishi kudumisha amani na ustawi wa michezo nchini
" Sheria ya Baraza la Michezo Tanzania Sura 105
Kifungu cha 4(1)(e): Serikali inaweza kuingilia masuala ya michezo pale inapohitajika kulinda amani, utulivu, na usalama wa taifa.
Kanuni za TFF (TFF 2022)
Kifungu cha 3(c): TFF inatakiwa kuhakikisha haki, usawa, na uwazi kwa vilabu vyote chini ya usimamizi wakena
Kifungu cha 73: Migogoro inapaswa kutatuliwa kwa haki kwa mujibu wa sheria za mpira, lakini bila upendeleo au vitisho",immesema sehemu ya taarifa ya andiko lake.
Amesema Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani(FIFA) inapinga serikali kuingilia moja kwa moja uendeshaji wa vyama vya mpira lakini hairuhusu ukiukwaji wa haki za msingi za klabu au mashabiki. Serikali inaruhusiwa kuhakikisha haki na usalama vinazingatiwa.
Hatua ya Serikali Haitakuwa Kuingilia TFF Moja kwa Moja
bali Kuitisha mazungumzo ya pande zote (Yanga, Simba, TFF, Bodi ya Ligi) kuweka meza ya maridhiano kupitia Baraza la Michezo (NSC).
kuangalia kama kweli kuna dhulma au ukiukwaji wa haki za kikanuni.
Amesema Serikali inaombwa iingilie kwa haraka ili isaidie TFF kupata suluhu ya haki
na itulize hisia za mamilioni ya mashabiki na isaidie kudhibiti mvutano kabla haujageuka machafuko ya kitaifa ikizingatiwa mwaka huu ni wa uchaguzi
