Wachimbaji wa Madini Kufikiwa na Benki ya NMB kwa Kuwezeshwa Mikopo

GEORGE MARATO TV
0


Na Shomari Binda-Musoma 

BENKI ya NMB imesema inazo fedha za kutosha na wanakwenda kuwafikia wachimbaji kuwapa mikopa na kuendesha shughuli zao za uchimbaji.

Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa Huduma za Wateja wa Mikopo ya Kati wa benki hiyo Dickson Richard wakati akitoa mada kwenye kongamano la maonyesho ya madini mkoa wa Mara kwenye ukumbi wa Mwembeni Complex leo juni 5,2025.

Amesema kwa sasa sekta hiyo ya madini inatambulika zaidi ikiwemo shughuli zake na zipo fedha wanazozitoa źa mikopo katika kuboresha kazi zao.

Katika kongamano hilo lililowashirikisha wachimbaji,wauzaji,wachenjuaji na wadau wengine meneja huyo amewaita kuchangamkia fursa hiyo kutoka benki ya kizalendo

Amesema fedha zipo na kikubwa ni kufuata taratibu zikiwemo taarifa sahihi ambazo zitapelekea kupata mikopo hiyo kwa haraka.

" Ndugu zangu benki ya NMB ni benki yenu na inazo fedha za kutosha kwaajili ya kutoa mikopo kwa wachimbaji na wadau wote wa sekta ya madini.

" Nimetoka makao makuu na hapa Musoma ni nyumbani nilianzia hapa miaka hiyo na nipo na wenzetu wa hapa mkoa wa Mara kuja kuwafikishia ujumbe huo kupitia kongamano hili la maonyesho ya madini mkoa wa Mara", amesema.

Kwa upande wao mameneja kutoka Wilaya zote za mkoa wa Mara wamesema wapo tayari kuwapokea wachimbaji na wadau wote wa sekta ya madini ili kuanza michakato ya utoaji mikopo hiyo.

Wamesema benki ya NMB inatambua mchango wa sekta ya madini na wapo tayari kuwapokea na kuwawezesha kwa mikopo pale watakakapowafikia.

Kwenye kongamano hilo wadau wa sekta ya madini pamoja na taasisi za kifedha ikiwemo benki ya NMB wamekuja na mapendekezo zikiwemo taarifa sahihi zitakazowezesha kupata mikopo.

Licha ya taarifa hizo ni wachimbaji kuhakikisha migao yao ya fedha za mgao wa uuzwaji wa madini ikiwemo dhahabu yanapitia benki.

Kongamano la maonyesho ya madini mkoa wa Mara yameingia siku ya pili hii leo ambapo kesho maonyesho hayo yatafungwa rasmi na Waziri zwa Madini Antony Mavunde kwenye uwanja wa shule ya msingi Mukendo





Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top