Na Shomari Binda-Musoma
WANACHAMA wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) wamekuja na maombi ya mabadiliko kuruhusiwa kupiga kura za maamuzi kuwachagua wabunge na madiwani.
Maombi hayo wameyatoa leo mei 22 2025 kwa nyakati tofauti nje ya kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Mara kilichofanyika makao makuu ya mkoa.
Wamesema mabadiliko ya kwanza ya kuongeza wigo wa wajumbe ni nazuri lakini kwa kuboresha waruhusiwe wanachama wote wenye kadi za Kielektroniki wapige kura hizo.
Mmoja wa wanachama hao aliyekitambulisha kwa jina la Baraka Mfungo kutoka Kata ya Kwangwa manispaa ya Musoma amesema wakiruhusiwa wanachsma wote itakuwa tiba sahihi ya kudhibiti Rushwa.
Amesema hakutakuwa na ugumu wowote wa upigaji kura hizo ikiwa utawekwa utaratibu mzuri kuanzia ngazi ya Kata.
Baraka amesema wao wamekuwa kama wametengwa wakati ni wanachama hivyo maombi yao ni kuruhusiwa kushiriki upigaji kura
Amesema vikao vya chama vya taifa vitakavyofanyika mwishoni mwa mwezi huu jijini Dodoma makao makuu ya chama kije na mabadiliko hayo.
" Jambo hili au ushauri huu uangaliwe kwa jicho la tatu maana licha kutoa fursa kwa wanachama wote litakuwa na tija.
" Wapo baadhi ya wanaotaka kutia nia wanadai wajumbe walioongezwa wanawamudu sasa ombi letu tupige kura hizi wanachama wote",amesema.
Kwa upande wake mwanachama Magoti Warioba mkazi wa Kijiji cha Murangi Musoma Vijijini aliyezungumza kwa njia ya simu na GMTV amesema anaona kuruhusiwa wanachama wote ni jambo jema linalopaswa kupitishwa.
Amesema Mwenyekiti wa Taifa wa chama ni msikivu hivyo atapokea maombi na kupitishwa kwa wanachama wote kupiga kura za maamuzi.
" Chama kwenye vikao vyake vya Taifa mei 29 na 30 kije na mabadiliko haya tunayoyaomba ili kila mwanachama aliye kwenye daftari na kadi ya Kielektroniki apige kura.
" Wasiachiwe watu wachache kufanya maamuzi ya wengi chama kije na ruhusa ya kila mwanachama amchague mgombea atakayeingia kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu wa ujumla oktoba mwaka huu",amesema.
Warioba Wambura mwanachama kutoka Tarime amesema wapo watia nia wanaosema wameandaa fungu la kuwamudu wajumbe hao.
Amesema kwanini wanachama wanatengwa na kuchukuliwa wajumbe wachache jambo ambalo halifai na ni kama vile wametengwa.
" Wasituone sisi tunafaa kwenye kura za jumla pekee huku kwenye maamuzi na maoni tunatengwa tunamuomba Mwenyekiti wa Taifa Mama yetu Dkt.Samia Suluhu Hassan na wajumbe kwenye vikao vinavyokuja waje na maamuzi haya",amesema.
"Kwanza tukipiga wanachama wote rushwa haitakuwepo pia chama kitajiweka sehemu nzuri ya ushindi maana tutakuwa tumefanya maamuzi wote kama tulivyofanya kwa wenyeviti wa vijiji na mitaa"alisema Mama Pendo
Wajumbe wa Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) wanatarajiwa kukutana mfei 29 na 30 Makao Makuu ya chama Dodoma kuzungumzia masuala mbalimbali ikiwemo kupitisha ilani ya uchaguzi wa 2025_2030






Comments
Post a Comment