Na Ada Ouko, Dodoma.
Ujumbe kwa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Masauni umetembelea bandari Oslo,Nchini Norway kwa lengo la kujifunza namna Bandari hiyo inavyohifadhi mazingira na kuzuia uzalishaji wa gesi joto.
Akizungumza na Ujumbe huo,Mkurugenzi Mkuu wa Bandari ya Oslo Ingvar Mathisen amesema kuwa ifikapo mwaka 2030, Bandari hiyo itakuwa imepunguza gesi joto kwa asilimia 85.
Mathisen ameueleza Ujumbe wa Tanzania kuwa Bandari ya Oslo ni bandari mtambuka na haizalishi gesi joto na kwamba Bandari hiyo ni ya tatu kwa ukubwa duniani kwa kuwa na teknolojia janja ya bahari.
Amesema kuwa lengo kuu la bandari hiyo ni kuhakikisha kuwa inapunguza gesi joto kwa 85% ifikapo mwaka 2030 ambapo Serikali ya Norway imeanzia kufikia lengo hilo kwa kutumia teknolojia.
"Kuanzia mwaka 2018,Bandari ya Oslo, Norway imeacha kupokea na kuendesha meli zake kwa kutumia mafuta, badala yake meli zote iwe za kisafirisha abiria, mizigo au starehe zote zinatumia umeme" Amesema Mathisen na kuongeza kuwa
"Hivyo kwa vyombo vyote ambavyo havitumii teknolojia hiyo, Bandari ya Oslo hutoza ada ya uzalishaji gesi joto-‘ Emission Fees’( inayo jumishwa kwenye mpango wa biashara ya Kaboni)"
Kupitia ziara hiyo Tanzania imebainisha fursa mbalimbali za uhifadhi na usimamizi wa Mazingira kupitia Uchumi wa Buluu na Biashara ya Kaboni.
Tanzania ni nchi ambayo Mashariki yake ina pwani ndefu ya bahari ya Hindi ambayo ina bandari kubwa za Dar es Salaam, Mtwara na Tanga.
Aidha kuna Bandari ndogo zinazohudumia Lindi, Kilwa Masoko, Mafia, Pangani na Kwale.
Bandari zote hizo hutumia vyombo vya usafirishaji ambapo Uwepo wa teknolojia ya kutambua kila chombo huzalisha kiasi gani cha gesi joto, Mamlaka husika kwa kushirikiana na Kituo cha Ufuatiliaji wa Kaboni - NCMC zinaweza kufanya biashara hiyo kwa kudai ada ya uzalishaji gesi joto.











Comments
Post a Comment