Ateta na mabinti wa mkoa wa wa kusini Unguja
Amwakilisha Mhe Wanu Hafidh Ameir (Mb) kwenye kongamano la Binti na Uongozi.
Mbunge wa Viti Maalum kundi la Vijana Taifa Mhe Ng'wasi Kamani amepata nafasi ya kushiriki kama Mgeni Rasmi katika kongamano la Binti na Uongozi lililoandaliwa na Senati ya Vyuo na vyuo Vikuu UVCCM Mkoa wa Kusini Unguja
Mbunge huyo wa vijana amemwakilisha mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa kusini Unguja Mhe Wanu Hafidh Ameir ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation inayofanya kazi kubwa ya kuwainua Mabinti na Vijana katika kukuza vipaji vyao vya uongozi, kiuchumi na kijamii.
Washiriki kwa kauli moja wameazimia kushiriki kikamilifu kwenye Uchaguzi Mkuu katika kampeni, kupiga kura na kupigiwa kura kwa nafasi mbalimbali, pamoja na kuhakikisha wanafuata nyayo za Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan- Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na viongozi wengi wanawake katika uthubutu, uchapakazi, umahiri, utulivu, uvumilivu, tabia njema na sifa zote kuu lukuki za kiuongozi.
Katika kuwaunga Mkono mabinti hao, Mhe Kamani amewachangia Tsh Milioni 2 ili waweze kuendeleza programu zao za uongozi.















Comments
Post a Comment