Kiongozi Chadema ainanga kauli mbiu ya kupinga uchaguzi akisema chama cha harakati kinajiandaa kujiua kisiasa

GEORGE MARATO TV
0

 

Kiongozi mwandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kutokea Tarime, mkoani Mara, Mohania Joseph Peter, amekianga chama hicho, akisema ni cha kiharakati na hakiwezi kufanya siasa.

Ndugu Mohania, ambaye amewahi kushika nafasi mbalimbali katika chama hicho ngazi ya mkoa, katika Baraza la Vijana wa Chama hicho (Bavicha), kabla ya kuwa msaidizi katika ofisi ya chama hicho Mkoa wa Mara, amesema chama kinachoendekeza harakati kinajiandaa kufa kisiasa na hakiwezi kuaminiwa kushika dola.

Kiongozi huyo amesema hayo, alipopewa nafasi ya kuzungumza kwenye mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, katika Uwanja wa Shamba la Bibi, mjini Tarime, leo Ijumaa tarehe 25 Aprili 2025, ambapo pia alitangaza uamuzi wa kuhama Chadema, akijiunga na CCM.

“Nimekuwa Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Mara. Nimekuwa Mwenyekiti wa Bavicha Jimbo la Tarime Vijijini. Lakini pia nimekuwa msaidizi wa ofisi ya Chadema mkoa. Kuna sababu mbili zilizofanya nimeamua kufanya maamuzi ya kuhama. 


“Unapokuwa kwenye chama cha siasa badala ya kuhimiza kushiriki uchaguzi, badala yake kinahimiza harakati, unaona chama hicho hakifai tena.Sababu ya pili, Chadema tangu kuanzishwa kwake ina miaka zaidi ya miaka 30 haijawahi kushinda nchi. Wanasema unayeshindana nae ukiona amekushinda, unaungana nae,” alisema Mohania.

Mbali ya Ndugu Mohania, wanachama wengine, wakiwemo viongozi wa vyama vya upinzani, ikiwa ni pamoja na Chadema, walijiunga na CCM kwenye mkutano huo, ambapo walipokelewa na Balozi Nchimbi, ambaye alisisitiza kuwa vifaa na vitendea kazi walivyovikabidhi kwake, atahakikisha vinarudishwa kwa sababu CCM haichukui vitu vya watu




Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top