Shule nyingine mpya ya sekondari yafunguliwa kata ya Mugango Musoma Vijijini

GEORGE MARATO TV
0

 

Na Shomari Binda-Musoma 

SHULE nyingine mpya ya sekondari ya Kumbukumbu ya Profesa David Masamba imefunguliwa na kukabidhiwa leo aprili 25,2025 kwa wananchi wa Kijiji cha Kurwaki Kata ya Mugango.

Hii inakuwa shule ya pili kufunguliwa kwenye jimbo hilo ndani ya siku 2 huku wananchi wakiishukuru serikali kwa kupata shule hiyo.

Akizungumza mara baada ya kuitembelea shule hiyo na kuikagua Mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka ametoa wito kwa wananchi kuilinda na kuitunza shule hiyo ili watoto waendelee kupata elimu.


Amesema jambo lingine ni kuhakikisha wanawapa ushirikiano walimu ili waendelea kufundisha na kuwa na ari ya ufundishaji na kuwataka wanafunzi kusoma kwa bidii.

Chikoka amesema wanaendelea kutoa asante na shukrani kwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kiasi cha shilingi milioni 584 kuunga nguvu za wananchi walioanza kuijenga shule hiyo.

Katika ujumbe wake kwa wananchi mkuu huyo wa Wilaya amesisitiza suala la chakula shuleni na hatamvumilia yoyote atakayekwamisha upatikanaji wa chakula shuleni.

Amesema Kata ya Mugango imekuwa ikifanya vizuri kwenye usimamizi wa elimu na kutaka kuendelea kukaza uzi na kuchukua tuzo za elimu ambazo zimeanzishwa.

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo amesema ni kiu yake kuona  maendeleo ya elimu yanafanikiwa.

Amesema kama mbunge ataendelea kusukuma maendeleo yakiwemo ya elimu na kudai mtu anayetaka uongozi apimwe kwa utendaji wake wa kazi.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Musoma Denis Ekwabi amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwaajili ya utekelezaji wa ilani wa miradi mbalimbali.


Amesema kwa mbunge Profesa Sospeter Muhongo amefanya kazi kubwa na yupo tayari kuendelea kufanya nae kazi kwa kipindi kingine.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top