Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Rajabu Mabele, ameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendeleza mafunzo ya vijana wa JKT.
Meja Jenerali Mabele, ameyasema hayo Aprili 17 mwaka 2025 alipokuwa anahitimisha mafunzo ya Awali ya kijeshi kwa vijana wa Operesheni miaka 60 ya Muungano katika kikosi Cha Ruvu JKT kilichopo mlandizi mkoani Pwani.
Meja Jenerali Mabele, amewaasa vijana hao kuzingatia Afya zao kwani afya ndio msingi na mtaji mkubwa kwa kijana wa Jeshi la Kujenga Taifa.
Naye Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda, Brigedia Jenerali Abubakar Charo, amewataka kwenda kuzingatia Mafunzo ya Stadi za Kazi na Stadi za Maisha kwani ndiyo yatakayowasaidia kujitegemea baafa ya kumaliza mkataba wa Jeshi la Kujenga Taifa.
Kamanda Kikosi Ruvu JKT Kanali Peter Mnyani akitoa taarifa fupi ya mafunzo amesema mafunzo hayo yalianza tarehe 30 Desemba 2024 na kuhitimishwa tarehe tarehe 17 Aprili 2025.