Wasira Apokelewa Sikonge, Awasilisha ujumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa Ccm

GEORGE MARATO TV
0


Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira amewasili wilayani Sikonge Mkoa wa Tabora na kushiriki mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM ya wilaya hiyo.

Wasira amewasili wilayani humo leo Aprili 17, 2025 akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 akiambata na viongozi mbalimbali wakiwemo baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora,  Said Nkumba.

Akizungumza na wana CCM katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya Chama Wilaya ya Sikonge, Wasira amesema pamoja na mambo mengine amefika kuwaeleza wanachama kuhusu uamuzi wa Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama kumchagua Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea urais wa CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka na mgombea mwenza wake ni Dk. Emmanuel Nchimbi.

Kwa upande wa urais wa Zanzibar, Wasira amewaambia wana CCM hao kuwa mkutano mkuu uliridhia na kumpitisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi kuwa mgombea wa CCM katika uchaguzi huo.










Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top