Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabiri Bakari katika kikao kazi na wajumbe kutoka Tume ya Utangazaji Zanzibar (ZBC) wakiongozwa na Katibu Mtendaji mpya wa Tume hiyo Ndugu Hijji D. Shajak, tarehe 15 Aprili, 2025, katika ofisi za TCRA Zanzibar.
Kikao hicho kimelenga kudumisha mashirikiano kati ya taasisi hizo mbili ili kuboresha Sekta ya Utangazaji.
Mnamo Septemba 15, 2023, TCRA na ZBC zilisaini mkataba wa maboresho (MoU) ya makubaliano ya kuboresha usikivu wa vituo vya redio vya Zanzibar katika mikoa ya Dar es Salaam na Tanga, na usikivu mzuri wa redio za mikoa hiyo kwa upande wa Zanzibar. Makubaliano hayo pia yalilenga kuongeza ushirikiano katika matumizi ya rasilimali masafa kwa ufanisi.