Na Shomari Binda-Musoma
MBUNGE wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo ametoa shukrani kwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi.
Shukrani hizo amezitoa wakati akichangia Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwenye Kikao cha 5 cha Bunge la 12 Mkutano wa 19.
Amesema kama mwakilishi wa wananchi wa jimbo la Musoma mjini anstoa shukrani nyingi kwa namna alivyowatendea mema kwenye kipindi cha uongozi wake
Akizungumzia suala la elimu amesema shule mpya 4 zimejengwa huku kila mmoja ikipata fedha zaidi ya milioni 500 na leo watoto wanasoma bila tatizo.
Amesema licha ya ujenzi wa shule mpya madara mengi mapya yameongezwa kwenye shule za zamani ambayo yamekuja kupunguza wanafunzi kujazana madarasani.
Mbunge huyo amesema changamoto ndogo ni mahala pa wanafunzi kukaa na kwa sasa kwa kutu.ia fedha zake na wadau wa elimu yanatengenezwa madawati zaidi ya 3500 ili kumaliza changamoto hiyo.
Kuhusu huduma za maji amesema upatikanaji ni asilimia 100 na kinachofanyika sasa ni kuhakikisha mwananchi atembei umbali wa mita 200 kufuata maji.
Huduma za afya amesema sio tatizo tena kwani kupitia zahanati,vituo vya afya na hospital wananchi wanapata huduma stahili.
" Mheshimiwa tupo hatua za mwisho kumaliza kipindi chetu cha miaka 5 kuwawakilisha wananchi na mimi kwa leo nijikite sana kuishukuru serikali chini ya Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa namna alivyotupatia fedha nyingi kutekeleza miradi ya maendeleo.
" Hatuna lawama kwa serikali kwani kuanzia kwenye elimu,afya,majj na hata miundombinu ya barabara tuko vizuri na kwa kweli tunamshukuru sana Rais Samia",amesema
Mbunge huyo amesema anachopigania na kuomba ni uchumi na wananchi kuwa na fedha mfukoni baada ya kukosekana kwa viwanda kwaajili ya kujishughulisha.
Amesema kupitia shughuli za uvuvi anaishukuru serikali kwa kuwezesha vikundi takribani 14 vizimba pamoja na boti na kuwasemea waliokuwa wafanyakazi wa kiwanda cha nguo cha Mutex kulipwa mafao yao baada ya kiwanda hicho kubinafsishwa.


Comments
Post a Comment