Kirigini Ampongeza Rais Dkt.Mwinyi Kusimamia Misingi Ya Uongozi qa Hayati Rais Abeid Amani Karume

GEORGE MARATO TV
0


Na Shomari Binda-Musoma 

RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt.Hussen Ally Mwinyi amepongezwa kwa kusimamia misingi ya uongozi uliofanywa na Hayati Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Sheikh Abeid Aman Karume.

Pongezi hizo zimetolewa na kada wa Chama cha Mapinduzi( CCM) na Mjumbe wa zamani wa (NEC) Paul Herman Kirigini.

Akizungumza kwa njia ya simu na GMTV leo aprili 7 katika kumbukizi ya miaka 53 tangu kifo cha Hayati Karume amesema moja ya misingi hiyo ni kuwaletea maendeleo wananchj wa Zanzibar.

Amesema tangu serikali ya awamu ya 8 ya Dkt.Mwinyi iingie madarakani yameshuhudiwa mabadiliko makubwa ya kimaendeleo kwenye visiwa vya Zanzibar.

Kirigini amesema moja ya kumbukumbu ya hutuba za Hayati Shekh Abed Aman Karume ni vijana kujiandaa kuja kuwaongoza wananchi na kuwaletea maendeleo wananchi jambo linalofanywa vyema na Rais Dkt.Mwinyi.

Amesema ujenzi wa skuli kwa ajili ya maendeleo ya elimu zimekuwa zikijengwa na kushuhudiwa ufunguzi wake mara kwa mara.

Kirigini pia amezungumzia miradi mingine mbalimbali ya maendeleo ya kiuchumi ambayo pia imeonekana ikifunguliwa na kuzinduliwa kwenye visiwa vya Zanzibar.

" Tunapomkumbuka leo Mzee wetu Hayati Rais Abed Aman Karume miaka 53 ya kifo chake tupongeze namna Rais Dkt.Hussen Ally Mwinyi anavyoishi na maono yake.

" Maendeleo kwa wananchi yalikuwa malengo ya Hayati Karume na leo tunashukuru tukiona leo mambo mazuri yanaonekana katika serikali ya Mapinduzi Zanzibar",amesema.

Aidha Kirigini ametoa wito kwa vijana na wanaopata nafasi ya kuaminiwa kwenye nafasi za uongozi kuzisimamia vyema na kuwaletea wananchi maendeleo.





Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top