Washitakiwa wanane wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera kwa mara ya kwanza kujibu mashtaka yanayowakabili ya uhujumu uchumi, ambapo walikamatwa wakiwa na madini ya bati yenye thamani ya zaidi ya milioni 18 bila kibali.
Raymond Kimbe ni wakili wa Serikali mwandamizi kwa kushirikiana na Alfred Tairo wakili wa Serikali na Duke Mwanguku Mwendesha mashitaka akisoma shauri hilo namba 6758/2025 yenye mashtaka matano yanayowakabili washitakiwa namba moja mpaka sita mbele ya hakimu mkazi mwandamizi Allen Ifunya.
Kimbe amesema washitakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa mnamo Februari 11 mwaka huu katika eneo la Mulongo Wilayani humo walikutwa na madini aina ya bati yenye uzito wa kilo 310 yenye thamani zaidi ya milioni 13 kinyume cha sheria
Washtakiwa hao ni Diana Dickson Antoni,Dickson Antoni,Deusi Daud,Benjamin Ernest, Alfred Ntiba na Brighton Sadiel ambao wanashitakiwa kwa makosa matano ikiwemo kuongoza genge la uharifu,kufanya biashara ya madini bila kibali,kukutwa na madini bila kibali,kufanyabiashara bila kibali na kusababishia mamlaka hasara ya shl.milioni moja zitokanazo na tozo na mirahaba.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo washitakiwa wote hawakutakiwa kujibu lolote kwasababu ofisi ya mwendesha mashitaka wa Serikali bado haijatoa kibali cha kusikilizwa kwa shauri hilo katika mahakama hiyo.
Wakati huohuo katika kesi ya pili kesi namba 6757/2025 inayowakabili Suzan Twaisige na Justus Chabona oliyosomwa mbele ya hakimu mfawidhi Fravian Kubingwa na Wakili Kimbe ambapo washitakiwa wanakabiliwa makosa matatu ikiwemo kukutwa na madini ya bati yenye thamani ya shil mil.5.7 mali ya Serikali bila kibali,kufanya biashara za madini bila kibali na kusababishia Serikali hasara ya shl 400,000
Washitakiwa wote kwa pamoja hawakutakiwa kujibu lolote na wote wanane wamerudishwa rumande kwasababu wameshindwa kukidhi masharti ya dhamana ambapo, washitakiwa sita wa kesi namba 6758 watafikishwa tena mahakamani Machi 31 na wawili wa kesi namba 6757/2025 watafikishwa tena Machi 28 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa kesi zote mbili.
Akizungumza nje ya mahakama hiyo kaimu afisa madini mkoa wa Kagera Nobart John amewataka wadau wote wanaohusika na sekta hiyo kufuata sheria na taratibu pale wanapojihusisha na biashara ya madini ili kuepukana na kukutwa na hatia pale wanapokwenda kinyume na sheria za nchi.









Comments
Post a Comment