Mwandishi wetu ;Dodoma
Wadau wa habari Tanzania wameipongeza Taasisi ya MISA Tan Kwa kuwa na uthubutu wa kuwaleta wadau wa habari katika kongamano la MISA Wadau Summit 2025 Jijini Dodoma.
Mwakilishi toka PSSSF Bwana Valentino Maganga alisema kuwa, Taasisi ya MISA imefanya jambo la kipekee Kwa kuandaa kongamano na kuwa na muda wa kujadili masuala ya kiuchumi.
Binafsi yetu kama PSSSF tunaamini kuwa, bila vyombo vya habari ni vigumu wananchi kuelewa wajibu wetu na kazi zetu.
Naye Mhandisi Andrew Kisaka amesema kuwa anaishukuru MISA Tan Kwa kutoa nafasi ya TCRA kutoa elimu ya kanuni za uchaguzi.
Naye Josephine Joseph toka TASAF alisema kuwa, anaishukuru MISA Tan Kwa kutoa nafasi ya kujadili maendeleo ya kiuchumi kupitia vyombo vya habari, hilo ni jambo zuri sana.
Naye Mwenyekiti wa MISA Tanzania Bwana Edwin Soko alisema kuwa, kongamano la MISA hilo ni mwendelezo wa jitihada za MISA kwenye kujenga mahusiano na wadau wa habari hapa Nchini.
MISA Wadau SUMMIT 2025 imefanyika Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na wadau wa habari wakiwemo, NSSF, PSSSF, TAKUKURU, TASHICO, THRDC na TCRA.

















Comments
Post a Comment