Na Michael Uled
Baada ya kukaa mtaani kwa miaka miwili bila KAZI,sikuwa na Option nyingine!Katika pita pita zangu niliona tangazo la ajira kutoka kampuni ya Uchimbaji Madini ya Shanta Gold Mining Tanzania!
Kumbuka nilikuwa mtaani nikiwa na Elimu yangu ya (Masters)lakini sikuwa na KAZI kwa miaka zaidi ya miwili au mitatu hivi Haikuwa rahisi!
Tangazo lile la KAZI la Shanta lilikuwa linahitaji watu wa (CCTV Camera Operative),wenye sifa mdogo ndogo kama kupitia kozi za JKT! Lakini pia sifa kuu ilikuwa ni kuwa Elimu angalau ya form four tu!Pamoja na kuwa na Elimu yangu ya Master Of Arts in Communication lakini sikusita kuomba!
ILIKUWA HIVI!👇🏿👇🏿
Nafasi ile ilikuwa inahitaji mtu mwenye Elimu ndogo tu ya Form four lakini pia mwenye "skills" za CCTV operation tu!
Baada ya kuomba KAZI ile ya "form Four" nilipata!Kwahiyo Degree zangu mbili nikaweka pembeni nikawa natumia cheti cha form four lakini huku nikiwa na Mshahara mzuri sana!Ajira nyingi kwa sasa zipo kwa watu wenye "skills" na sio watu wenye "Degree"moja au mbili!
Ndio hapo WAZO na maelekezo ya Mh Waziri Mkuu Majaliwa yana "matter" sana!Ukiwa na "skills" toka "VETA" huku ukiwa na "Degree" yao inakuwa rahisi sana kupata ajira!Ajira nyingi kwa sasa zipo kwa watu wenye "skills" ndogo ndogo na zinalipa sana!
Imagine!CCTV Camera Operative ambaye ni form four pale kampuni ya kuchimba Madini ya Geita Gold Mining analipwa kati ya 1.8 milioni mpaka 2.2M kwa mwezi!Skills hizo ndogo ndogo zinapatikana VETA tu!
Nimeona mitandaoni "wasomi" wakipinga kauli ya Mh Waziri Mkuu Majaliwa!Waziri Mkuu hawezi kukurupuka akaja na kauli ambayo hajaifanyia "research"!Serikali inafahamu kuwa fursa nyingi za ajira zipo kwenye "skills" ndogo ndogo!
Endeleeni kukaa na "Degree" zenu majumbani!Ajira nyingi sasa hivi (70%)mfano kwenye sekta ya Uchimbaji wa Madini zimezibwa na wahitimu kutoka VETA!
Ni muhimu sana vijana wahitimu wa Shahada za Vyuo Vikuu wakangamua kauli ya Waziri Mkuu Majaliwa!
George Michael Uledi!

Comments
Post a Comment