Na Shomari Binda-Musoma
MKUU wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka amezindua utoaji wa huduma za afya kwenye kituo kipya cha afya cha Kata ya Makojo chenye Vijiji 3 vya Chimati, Chitare na Makojo)
Jimbo la Musoma Vijijini linaendelea kuboresha na kuimarisha utoaji wa huduma za afya ndani ya Kata zake 21 zenye jumla ya vijiji 68.
Akizungumza jana machi 6/ 2025 wakati wa uzinduzi huo mkuu huyo wa Wilaya amesema suala la afya kwa wananchi ni suala la msingi kwani afya bora inamfanya mwananchi kutekeleza vyema majukumu yake.
Amesema serekali ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imekuwa ikifanya jitihada kubwa kuboresha utoaji wa huduma za afya na Musoma Vijijini imekuwa ikifikiwa na huduma hizo.
Chikoka amesema watoa huduma wanapaswa kuzingatia maadili ya utoaji huduma nzuri kwa wananchi kuanzia kwenye zahanati,vituo vya afya na hospital.
Amesema sio vyema kuona wananchi wakilalamikia huduma wakati serikali imejenga kituo cha afya na kupeleka vifaa tiba na dawa.
Kwa upande wa taarifa iliyotolewa leo machi 7 2025 na ofisi ya mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo imesema jimbo hilo licha ya kuwa na zahanati na vituo vya afya ina hospital ya Halmashauri yenye vifaa vya kisasa vya matibabu ikiwemo complete radiology unit (mobile digital X-ray),static X-ray), oxygen-production plant, na two ultrasound machines.
Vituo 6 vya afya vilivyopo vikiwa na vifaa tiba vya kisasa ni pamoja na Bugwema, Kiriba, Kisiwa cha Rukuba, Makojo, Mugango na Murangi
Kwa mujibu wa taarifa hiyo zahanati 26 za Serikali na 4 za binafsi zipo zinatoa huduma wakati zahanati 17 mpya zinajengwa kwa nguvu za wananchi na nyingine zimeanza kupokea misaada ya kifedha kutoka serikalini.
" Magari ya wagonjwa 7 likiwemo gari kubwa la kisasa kutoka Japan (lenye vifaa vya upasuaji) ambalo liko kwenye kituo cha afya cha Murangi yanatoa huduma
"Ambulances 7 zipo (Kwikonero (Hospitali ya Halmashauri),Masinono (Kata ya Bugwema), Kurugee (Kata ya Bukumi)
,Murangi (Kata ya Murangi),Rusoli (Kata ya Rusoli),Nyang'oma (Kata ya Mugango)na Nyasurura (Kata ya Ifulifu)" imesema taarifa hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo alitoa Ambulances tano (5) kati ya hizo saba (7) zilizoko jimboni



Comments
Post a Comment