Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Mara (RCC) leo tarehe 03/3/2025 imekubaliana kwa kauli moja kuligawa jimbo la uchaguzi la Serengeti ili kupata majimbo mawili ya Serengeti Mashariki na Serengeti Magharibi.
Wakitoa hoja kuhusu mgawanyo wa jimbo hilo, wachangiaji wote wamezungumzia kuhusu ukubwa wa jimbo hilo lenye kata 30 na kubeba asilimia kubwa ya eneo la Mkoa wa Mara.
Hoja hiyo imejadiliwa baada ya kupitishwa kwenye vikao vya kisheria vya ngazi za Wilaya na Halmashauri na baada ya kupitishwa kwenye RCC suala hilo litawasilishwa Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania (INEC) kwa ajili ya maamuzi.
Agenda nyingine zilizojadiliwa katika kikao hicho ni mapendekezo ya mpango na bajeti ya Sekrerieti ya Mkoa wa Mara na Mamlaka za Serikali za Mitaa, bajeti ya maendeleo ya sekta ya maji na nishati.





Comments
Post a Comment