Na Shomari Binda-Musoma
Kongamano kubwa la mijadala ya uboreshaji na ufundishaji kujenga uelewa kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari litafanyika kwa siku 3 jimbo la Musoma vijijini.
Wataalamu wa elimu watakaoongoza kongamano hilo litakalofanyika machi 25 hadi 27 jimboni humo ni Dr. Zablon Kengera kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM),Dr. George Kaangwa, UDSM na Jeff Makongo mtaalam wa ubunifu (Ubunifu Associates)
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo februari 28/2025,Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof.Sospeter Muhongo atagharamia kongamano hilo kwa siku hizo tatu.
Taarifa hiyo imedai mjadala wa kwanza utafanyika machi 25 Mwaka huu kwenye shule ya sekondari ya Busambara ambapo washiriki watakuwa maafisa elimu Kata 21 wataalam na wadau wengine wa elimu
Mjadala wa pili utafanyika machi 26 kwenye shule ya msingi Busambara kuanzia saa tatu za asubuhi hadi Saa sita za mchana hyku washiriki wakiwa walimu wakuu 120 na wataalamu watatu na baadaye kuanzia saa nane mchana hadi Saa 11 jioni,kongamano litaangazia elimu ya Sekondari ,washiriki wakiwa wakuu wa sekondari 32 na wataalam watu.
Siku ya mwisho machi 27 Mwaka huu,mjadala utafanyika makao makuu ya Halmashauri ya wilaya Musoma yaliyopo Suguti Kwikonero.
Washiriki wakiongozwa na mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri,Maafisa elimi,madiwani,mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini,Profesa Sospeter Muhongo,wataalamu watatu pamoja na washiriki kutoka kwenye shule za serikali na binafsi.
Mijadala ya miaka ya nyuma
mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini amekuwa akifadhili mijadala yenye malengo kuimarisha sekta ya elimu ikiwemo mjadala wa mkoa wa Mara mwaka 2019 pamoja na mjadala wa wakuu wa sekondari za Musoma Mwaka 2021.
Aidha taarifa hiyo imewaomba wadau wa elimu kuendelea kuchangia kuboresha sekta hiyo kwenye jimbo la Musoma vijijini.

Comments
Post a Comment