Mbunge Mathayo azungumzia Mafanikio Utekelezaji wa ilani ya Ccm Jimbo la Musoma Mjini Mbele ya Wasira

GEORGE MARATO TV
0



Na Shomari Binda-Musoma 

MBUNGE wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo amezungumzia utekelezaji wa ilank ya uchaguzi ya CCM mbele ya Makamu Mwenyekiti wa chama hicho taifa Stephine Wasira.

Akizungumza kwenye ukumbi wa mikutano wa chama hicho zilizopo kẁenye ofisi za mkoa ikiwa ni muendelezo wa ziara ya makamu huyo wa chama amesema utekelezaji wa miradi ya maendeleo umetekelezwa ipasavyo.

Amesema kwenye sekta ya elimu ilani imetekelezwa ikiwa ni pamoja na kujengwa kwa shule mpya na kupelekea kila mtoto anayetakiwa kwenda shule anapata nafasi hiyo.

Mathayo amesema elimu ndio suala la msingi na kwa jimbo la Musoma mjini hawana deni na Rais Dkt.Ssmia Suluhu Hassan bali yeye ndio anawadai kumpa kura za kishindo kwenye uchaguzi sa mwaka 2025.

Amesema licha ya utekelezwaji wa ilani suala la kiuchumi kwa wananchi bado ni changamoto kutokana na viwanda kufa na kumuomba Makamu Mwenyekiti kusaidia eneo hilo.

 " Tunakupongeza Makamu Mwenyekiti kwa kuchaguliwa kwenye nafasi hiyo na tunakukaribisha Musoma mjini maana hapa ni nyumbani kwako.

" Utekelezaji wa ilani umetekelezwa kwa ufanisi kwenye miradi mbalimbali  na eneo tunalo lipigania kwa sasa ni uchumi wa wananchi",amesema.

Akizungumza na wanachama wa CCM Musoma mjini,Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa Stephine Wasira amewapongeza wanachama kwa mapokezi yao makubwa kwa kujitokeza kwa wingi.

Amesema viwanda kwa Musoma mjini vikiwemo vya samaki vimekufa kutokana na kukosekana kwa samaki na kupelekea uchumi kushuka.

Amesema upotevu wa samaki umetokana na wavuvi kuvua hadi maeneo ya mazalia na kudai jitihada zinaendelea kufanyika ili kuboresha eneo hilo na mengine kuinua uchumi.

Aidha Wasira amesisitiza viongozi wa CCM kuendelea kuwasikiliza watu kwenye maeneo yao na kufanikisha kutatua matatizo yao ili kuaminiwa zaidi na kushika dola.

Mwenyekiti wa  CCM Wilaya ya Musoma mjini Benedict Magiri akitoa shukrani za chxma zmesema watayafanyia kazi maelekezo yaliyotolewa ikiwa ni pamoja na kuwasikiliza watu.










Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top