KIKUNDI cha wazaliwa tarafa ya Kiagata wachangia vifaa vya ufundishaji sekondari ya Kiagata

GEORGE MARATO TV
0


Na Shomari Binda-Butiama

KIKUNDI cha wananchi wakazi wa Tarafa ya Kiagata wilayani Butiama wamechangia vifaa vya ufundishaji ikiwemo mashine ya kudurufu karatasi yenye thamani ya shilingi milioni tatu na laki tano kwenye sekondari kongwe ya Kiagata katika tarafa hiyo.

Wakazi hao wamechangia vifaa hivyo kupitia michango ya wanakikundi cha WhatsApp cha Kiagata Zone huku wito ukitolewa kwa jamii kurudi nyumbani na kuchangia masuala ya maendeleo.

Akizungumza mara  baada ya kukabidhi vifaa hivyo Mwenyekiti wa kikundi hicho Robert Silyvester Maganya amesema jamii haipaswi kuiachia serikali katika kuchangia mambo ya jamii yakiwemo ya maendeleo katika vijiji walivyozaliwa,kupata elimu na kuwafanya watambukike nje ya maeneo ya vijiji hivyo.

Amesema kama sehemu ya jamii na wazawa wa tarafa ya Kiagata wameamua kurudi nyumbani na kuchangia sekta ya elimu  na miradi mingine katika jamii ya tarafa hiyo.

Amesema baada ya kusikia changamoto ya kudurufu karatasi kwenye shule hiyo walijichangisha na kupata mashine na kuipeleka kwenye shule hiyo ili iweze kutatua tatizo hilo.

Robert amesema elimu ni suala muhimu na yenye manufaa kwa jamii hivyo kuweka mazingira mazuri ya ufundishaji uleta mafanikio. 

" Kupitia kikundi chetu tumejichangisha nakuja kusaidia nyumbani kwenye sehemu hiyo kwa wakati mwingine tutakapojaaliwa tutakuja kuchangia kwenye eneo lingine.

" Kikubwa ni jamii kuwa na utaratibu wa kurudi nyumbani na kuchangia mambo ya jamii na sio vyema kuiachia serikali peke yake",amesema.

Kwa upande wake mkuu wa shule ya sekondari Kkiagata Daudi Marwa akitoa shukrani kwa kikundi hicho amesema kuwa ujio wa mashine hiyo ya kudurufu karatasi itachangia kukuza ufaulu mkubwa shuleni hapo kwani mashine iliyokuwepo ilifanya kazi Kwa kusuasua na kulipunguza kasi kufanyika Kwa mitihani ya majaribio.

 Amesema kutokana na hali hiyo iliwalazimu kusafiri umbali mrefu kuipata huduma hiyo na kwa gharama kubwa.

Afisa Elimu Kata ya Nyamimange Bandiho Byarugaba,amesema kuwa kuna uhitaji mkubwa wa mashine za kudurufu au kuchapisha mitihani katika shule hizo na kupatikana kutachangia maendeleo mazuri ya wanafunzi kitaaluma katika wilaya ya Butiama.

Kwa upande wao wanafunzi wa shule hiyo wamekishukuru kikundi hicho kwa msaada waliowapatia ambao unakwenda kuwasaidia kwenye maendeleo yao ya kielimu. 











Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top