Wasira-hatuko Tayari Chadema Waje na azimio Ya Kuvunja Sheria za Nchi

GEORGE MARATO TV
0


  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama wa Chamapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amesema Chama na serikali yake haitakubaliana na azimio lolote litakalotolewa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya kukutana kwa faragha kama walivyotangaza viongozi wa chama hicho, juzi.

Amesema amesikia chama hicho kikitangaza kwamba kinakwenda kujifungia kisha kije na jambo ambalo halijapata kushuhudiwa nchini, hivyo ametoa angalizo jambo hilo ni lazima lifuate sharia za nchi.

Wasira amesema hayo leo alipohutubia wananchi katika mkutano uliotumika kuzindua sherehe za maadhimisho ya miaka 48 ya kuzaliwa kwa Chama kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Stendi ya Zamani mjini Bunda.

“Wamesema wanajifungia halafu waje wafanye jambo ambalo halijapata kuonekana, nikasema ni jambo gani, mimi nikaona huko kujifungia ile ni honeymoon maana honeymoon simnaijua, watu wakishaoana wanajifungia mahali…ile ni honemoon.

“Tunawaambia tunawatakia heri kwenye honeymoon lakini tunawaambia lolote watakalotoka nalo kwenye honeymoon lazima lifuate sheria, waklija na honeymoon inavunja amani hatuwezi kuwaunga mkono.

Mapema baada ya kuwasili wilayani Bunda kwa mara kwanza tangu achagukiwe kwenye wadhifa huo,mzee Wasira amepata mapokezi makubwa yalipombwa waendesha bodaboda,bajaj na magari zaidi ya mia moja.

Baada ya kupokelewa na viongozi wa mkoa wa Mara wakiongozwa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara Patrick Chandi,alifika ofisi ya ccm wikaya na kufanya mazungunzo na kamati ya siasa ya wilaya kabla ya kuhutubia mkutano huo ambao uliudhuriwa na maelfu ya wananchi wa wilaya ya Bunda.






Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top