Wananchi wa Mkoa wa Kagera wametakiwa Kuachana na Imani Potofu

GEORGE MARATO TV
0


 Na Angela Sebastian ;Bukoba

Mkuu wa mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa amewataka wananchi wa mkoa huo kuepukana na imani potofu na za kishirikiana ili kuwezesha kudhibiti kwa kiasi kikubwa  mlipuko wa ugonjwa wa marburg ambao ni hatari na haujapata tiba ya moja kwa moja na kunusuru kuenea kwa kiwango kikubwa.

Mwassa ameeleza hayo leo wakati wa mafunzo ya siku moja  kwa waandishi  wa habari zaidi ya 100 wa  vyombo mbalimbali ili wapate elimu juu ya kuandika habari sahii,wapate wapi taarifa sahii zisizozua taaruki katika jamii juu ya mlipuko wa ugonjwa wa marburg yaliyoandaliwa na Wizara ya Afya na wadau mbalimbali.

"Wananchi wengi hawaamini na wanapuuza kila kinachosemwa na wataalam,Watanzania tuna hulka ya kutoamini jambo hasa pale tunaposikia aliyeambukizwa ni mmoja au kufa ni mmoja yaani sisi kuamini kwetu ni mpaka wawe wamekufa wengi hii ni fikra potofu tena wengine wanafananisha na imani za kishirikiana tuache tufuate maelekezo yanayotolewa na wataalam"Rc Mwassa 

Amesema busara ni kukinga na siyo kusubiri kutibu, siyo  kusubiri watu watu wadondoke bali kuwaelimisha watu wajikinge kabla hivyo akawataka waandishi kuhakikisha wanatoa elimu kwa ĵamii kupitia vyombo vyao vya habari jinsi ya kuchukua tahadhari na kujikinga na ugonjwa huu, hatari ambapo ametoa mfano kuwa wakiugua watu 10 tisa kati yao hufari.

Amesema hivyo tunahitaji nguvu kubwa katika kufanya kampeni juu ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko kama huu wa marburg pindi yanapotokea. 

Amesema kuwa Marburg ilitangazwa rasmi na Rais Dk Samia Suluhu Hassan mnamo tarehe 20 mwezi huu na kusema kuwa kipo kisa cha mtu mmoja  ambacho kimetokea wilayani Biharamulo hari ambayo imesababisha timu ya Serikali kupitia idara ya Afya na wadau mbalimbali kufika Wilayani humo na kuanza kuchukua hatua madhubuti ili kuhakikisha ugonjwa huo hausambai na kuleta visa vipya.

Naye Mkurugenzi wa kinga toka Wizara ya Afya Dk. Ntuli Kapologwe ametaja dalili za ugonjwa huo kuwa ni homa,maumivu ya kuchwa,maumivu ya misuli,kuharisha,mwili kuishiwa nguvu,vidonda vya koo,vipelele vya ngozi,maumivu ya tumbo,kutapika ,kutokwa damu sehemu mbalimbali za wazi mfano puani,kutapika damu na kuharisha damu.

Naye dk.Norman Jonas ni mratibu wa huduma za Afya ngazi ya jamii kutoka Wizara ya Afya alimesema ugonjwa wa marburg unasababishwa na virusi vya marburg na unaambukizwa kwa haraka kwa njia mbili ambazo ni kutoka kwa  wanayama na kwa binadamu na binadamu kwenda kwa binadamu.

Jonasi amesema unaenea kwa njia zifuatazo kugusa majimaji ya mwili kama vile kinyesi,matapishi,jasho,,mkojo na damu pia vyombo,magodoro na nguo,kula au kugusa mizoga au wanayama walioambukizwa mfano popo,nyani,tumbuli na sokwe.

Naye mwakilishi kutoka Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani(UNICEF)  Dkt. Edna Moturi ameishukuru Serikali kwa kuendelea kushirikiana na wadau katika mapambano ya ugonjwa wa Marburg kwa jamii hivyo kwa kushirikiana na Serikali wataendeleza Mafunzo kwa makundi mbalimbali  ya kijamii ikiwemo Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii, Waganga wa Tiba Asili, Bodaboda na makundi mengine.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top