Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Miaka 65 ya Maisha ya Rais Samia, Safari yake Ya Kusisimua Kutoka Karani Masijala Hadi Mkuu wa Nchi


Na Bwanku M Bwanku.

Leo Januari 27, 2025 Taifa letu linasherehekea miaka 65 toka kuzaliwa kwa Rais wa sasa wa Awamu ya 6 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, anayehudumu kwa mara ya kwanza kwenye nyadhifa ya juu kabisa nchini toka achukue mikoba hiyo Machi 19, 2021 baada ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya 5 Hayati John Pombe Magufuli.

Kwa wasiyemfahamu sana, Rais Samia, ndiye Mwanamke wa kwanza katika historia ya Tanzania kushika nafasi ya Urais wa Tanzania baada ya pia kuwa Mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya Makamu wa Rais mwaka 2015 hadi 2021, nafasi kuu za juu kabisa katika Taifa letu.

Rais Samia Suluhu Hassan alizaliwa Januari 27, 1960 katika Kijiji cha Kizimkazi kilichopo Jimbo la Makunduchi, Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja Visiwani Zanzibar, kabla ya kuanza masomo yake ya Msingi katika shule mbalimbali ikiwemo Shule ya Msingi Chwaka kuanzia mwaka 1966 hadi 1968, kisha Ziwani mwaka 1970 na baadae Shule ya Msingi Mahonda mwaka 1972.

Baadae akajiunga Sekondari ya Ng'ambo kwa masomo ya kidato cha kwanza hadi cha tatu kisha Shule ya Sekondari Lumumba alikomaliza Kidato cha nne mwaka 1976. 

Kwa maelezo yake mwenyewe Rais Samia wakati akihojiwa na Kituo cha Habari cha TBC, kuanzia Shule ya Awali mpaka anafika Kidato cha nne alisoma kwenye shule zaidi ya 10 na anataja sababu ya hiyo kutokea ni kwasababu Baba yake Mzazi alikuwa Mwalimu kwahiyo alipokuwa anahamishwa kwenye vituo vya kazi na yeye alihama na familia yake kwenda kwenye Shule au eneo alilohamishiwa Baba yake.

Kwa mara ya kwanza Rais Samia anasimulia aliajiriwa mwaka 1977 katika Ofisi moja ya kwenye Wizara ya Mipango na Maendeleo- Zanzibar akiwa na umri mdogo sana wa miaka 17 lakini alirudishwa nyumbani baada ya kuonekana kuwa na umri mdogo lakini baadae aliitwa tena kufanya kazi eneo hilo na ndiyo ilikuwa ajira yake ya kwanza na mwanzo wa safari yake ya Utumishi wake katika Ofisi hiyo ya Maendeleo. 

Baadae alijiendeleza kimasomo kwa kusoma Ngazi ya Cheti (Certificate) alipohitimu mwaka 1983 kwenye masuala ya Uchumi na Takwimu kwenye Chuo cha Uchumi Zanzibar na ndipo alipoajiriwa kufanya kazi kwenye Wizara ya Mipango na Maendeleo mwaka 1983 hadi 1986 na baadae kwenda Chuo Cha Maendeleo ya Uongozi Mzumbe (IDM) kufanya Advanced Certificate ya Utawala, kabla ya kwenda kusoma Kozi ndogondogo za miezi mitatu mitatu kwenye Chuo cha Utawala wa Umma kule Lahore, Pakistan mwaka 1987, kisha Taasisi ya Eastern and Southern African Management Institute (ESAMI) mwaka 1991 na Taasisi ya Uongozi ya Hyderabad, India mwaka 1998 kwa ajili ya Astashahada ya Utawala.

Baadaye, alikwenda sasa Chuo Kikuu cha Manchester, Uingereza alikosoma Undergraduate Diploma ya Uchumi kisha akafanya Masters Degree (Uzamili) kwenye Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Southern New Hampshire, Marekani.

Kama nilivyoanza kueleza pale juu kidogo, mwaka 1977 aliajiriwa akiwa Karani Masijala lakini kwa maelezo yake mwenyewe, aliona pale sio mahali pake maana alikuwa anafanya kazi zaidi ya aliowakuta pale kwa kufanya hata zile zilizofanywa na watu wa Juu wenye vitengo na ndio maana akaamua kwenda kuongeza elimu ili aendelee zaidi na baada ya kuongeza elimu kama nilivyoeleza pale Juu ndipo akaajiriwa na Shirika la Chakula Duniani (World Food Program) kwenye project zao mbalimbali pale Zanzibar, akafanya hapo kazi kwa miaka 9 kuanzia mwaka 1988 hadi 1997.

Baada ya kutoka Umoja wa Mataifa kwenye Shirika la Chakula Duniani, akaingia sasa kwenye Taasisi zisizo za Kiserikali (NGO's) akafanya kazi kubwa sana kuziendeleza ukuzaji wake wa NGOs za Zanzibar mpaka kuwa Mkurugenzi wa kwanza wa Taasisi zisizo za Kiserikali Zanzibar (ANGOZA) mwaka 1995 mpaka mwaka 2000 huku akifanya shughuli zingine mbalimbali na kushika nafasi zingine kama Mlezi wa Jumuiya ya Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Zanzibar kutoka mwaka 1997 hadi 2000, Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Fursa sawa kwa wote- EOTF kutoka 1996 hadi 2000, Mwanachama wa Lions Club Zanzibar kutoka 1991 hadi 1998, Mjumbe wa Kamati ya Uundaji wa Sera ya Elimu Zanzibar mwaka 1996, Mwanachama Mwanzilishi wa Taasisi ya Kuchochea Maendeleo ya Wanawake Zanzibar kutoka 1991 hadi 1994 na nafasi zingine kama Mjumbe wa Kamati ya Msamaha wa Wafungwa (Parole Committe).

Baada ya safari yote ya elimu ndani na nje ya nchi, kuzunguka kote huko na kufanya kazi kubwa na nzito kwenye Serikali, Taasisi za Kimataifa, NGO's na Taasisi zingine, hatimaye mwaka 2000 ndipo akapata mawazo ya kuingia kwenye Siasa na sababu moja tu anasema iliyomvuta kuingia kwenye Siasa, ni kwamba alikuwa anaangalia Baraza la Wawakilishi ile mijadala inavyoendelea, kama inavyofahamika Zanzibar upinzani umepamba moto kwahiyo kilichomsukuma ni kuingia tu kule nikasaidie kupeleka hoja za Wananchi na kuisimamia Serikali.

Mwaka 2000 akajitosa kwenye Siasa na kufanikiwa kushinda kuwa Mbunge wa Viti Maalum vya Wanawake baada ya watu wengi kwenye Mkoa wake wa Kusini Unguja kumkubali sana baada ya kazi kubwa aliyoifanya ya kuwasaidia Wananchi wakati akiwa na Shirika la Chakula Duniani kusaidia masuala ya chakula kwa wingi kwenye eneo hilo baada ya kuwa na uhaba wa chakula, akaingia Baraza la Wawakilishi na Rais wa Zanzibar wa wakati huo Mhe. Abeid Amani Karume akamteua kuwa Waziri katika Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira, Maendeleo ya Wanawake na Watoto kwenye Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ambako alifanya kazi kwa miaka mitano mpaka 2005 ambapo tena Wananchi waliendelea kumuamini kuwa Mbunge wa Viti Maalum na kisha tena 2005, Rais Karume akaendelea kumuamini na kumteua kuwa Waziri kwenye Wizara ya Utalii, Biashara na Uwekezaji ambako nako alihudumu kwa miaka mitano bila kubadilishwa wala kutumbuliwa mpaka 2010.

2010 kwenye Uchaguzi Mkuu akaamua kuachana na Ubunge wa Viti Maalum na kwenda kugombea Ubunge wa Jimbo kwenye Jimbo la nyumbani Makunduchi na kushinda kama kawaida yake na sasa kuwa Mbunge wa Jimbo na si tena wa Viti Maalum na kuingia moja kwa moja kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sasa akateuliwa kuwa Waziri kwenye Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia masuala ya Muungano mpaka mwaka 2015.

Mwaka 2014 wakati Taifa likipambana kupata Katiba Mpya na Rais wa kipindi hicho wa Awamu ya 4 Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kuunda Bunge Maalum la Katiba. Bunge la nyumbani la Wawakilishi la Zanzibar likampendekeza kuwa Msaidizi wa Bunge la Katiba na hivyo yeye kuteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Katiba na Hayati Samwel Sitta ambaye alikuwa Spika wa Bunge la Tanzania akiwa Mwenyekiti wa Bunge lile la Katiba. 

Ilipofika mwaka 2015 wakati Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikimsimamisha Hayati John Pombe Magufuli kuwa Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Kamati Kuu ya CCM chini ya Mgombea mwenyewe wa CCM Hayati Dkt. John Pombe Magufuli walimteua yeye kuwa Mgombea Mwenza wa Mgombea Urais wa CCM na baada ya CCM kushinda kwenye Uchaguzi Mkuu ule wa mwaka 2015 ulimfanya yeye moja kwa moja kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania chini ya Hayati Magufuli, akiwa Mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo ya juu ya pili kwenye uongozi wa nchi yetu kabla ya Machi 17, 2021 ambapo aliyekuwa Rais, Hayati Magufuli alipofariki dunia na yeye kuwa rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mpaka sasa, Tanzania ikisherehekea miaka 65 ya maisha yake toka kuzaliwa mwaka 1960, maisha ya Rais Samia Suluhu Hassan yamekuwa ya Utumishi tosha kwa watu huku akifanya kazi nyingi sana ndani ya nchi kwenye Taasisi zisizo za Kiserikali, ndani ya Serikali kwenye nyadhifa kubwa kubwa na nzito Kitaifa pamoja na kazi kubwa alizozifanya Nje ya Nchi hasa kwenye Shirika la Chakula Duniani.

Maisha yake yamekuwa msisimko tosha, darasa na inspirational tosha kwa watoto wa kike na Wanawake kuamini kwamba Wanawake ni Jeshi kubwa na kwa vijana kuamini kwamba kila kitu kinawezekana chini ya jua iwe umetoka kwenye familia maskini, uwe wa Jinsia yoyote ile na mengine, muhimu ni kuweka malengo yako na kufanya kazi kwa bidii na kujituma. Historia yake imejaa upekee na uimara wa Wanawake kwani licha ya yote lakini Rais Samia ameweza kuhimili mpaka sasa akiwa Mkuu wa Nchi iliyotoka kwenye majanga ya kuondokewa na Mkuu wake wa nchi na majanga ya maradhi ya Uviko-19 lakini bado Taifa liko imara.

Kwenye Chama chake cha siasa (CCM) ambacho ni moja ya Chama kikubwa kabisa cha Siasa Barani Afrika na Duniani kwa ujumla, Rais Samia ameshika nafasi nyeti sana na za juu kabisa kabla ya sasa yeye mwenyewe akiwa ndiye Mkuu wa Chama kama Mwenyekiti wa Chama hicho. Amepita kwenye nafasi mbalimbali nyingi na kubwa sana ndani ya Chama toka ajiunge nacho mwaka Juni 10, 1987.

Ndani ya CCM, Rais Samia kabla ya sasa kuwa Mkuu wa Chama hicho kama Mwenyekiti, amewahi pia kushika nafasi za juu kabisa ndani ya Chama ambazo zingine anaendelea kuzishika mpaka leo kama kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, nyadhifa alizonazo mpaka sasa. Nyadhifa hizi ni za juu sana na zote zikiwa ndizo zenye maamuzi ndani ya CCM.

Pia amewahi kuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja, Mjumbe wa Kamati za Siasa Mkoa na Wilaya ya Kusini Unguja, Mwanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) na zaidi kushiriki kwenye tukio muhimu na nyeti la kuandika Ilani ya CCM mara 4 mfululizo kuanzia mwaka 2005/2010, 2010/2015, 2015/2020, 2020/2025.

Toka ashike usukani wa kuliongoza Taifa amefanya mageuzi makubwa sana ya maendeleo ikiwemo uendelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo, kushusha fedha za miradi kila mahali na mengine mengi. 

Akiwa na miaka mitatu pekee katika uongozi, tayali Rais Samia ametunukiwa Shahada 4 za Heshima (Honoris Causa) na Vyuo Vikuu mbalimbali ndani na nje ya nchi. Walianza UDSM Novemba 30, 2022 kumtunuku Shahada ya Juu ya Heshima kwenye Humanitia na Sayansi Jamii (Social sciences), Oktoba 10, 2023 wakafuata Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru cha nchini India na wiki hii Desemba 28, 2023 Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA) kumtunuku Shahada nyingine ya Uzamivu ya Usimamizi wa Utalii na Masoko (Doctor of Philosophy in Tourism Management and Marketing- Honors Causa) na kisha Chuo Kikuu kikubwa cha Ankara cha nchini Uturuki kumtunuku tena Rais Samia Udaktari wa Heshima.

Si jambo linalotokea mara nyingi kwa kiongozi mmoja ndani ya Taifa kutunukiwa Shahada 4 za Heshima kwa mpigo ndani ya muda mfupi wa uongozi wake. Wote tunakumbuka Hayati Rais Magufuli wakati wa uongozi wake wa Awamu ya 5 alitunukiwa mara moja Shahada ya Heshima na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) mwaka 2019 na Mstaafu Rais wa Awamu ya 4 Jakaya Kikwete pia mwaka 2011 alitunukiwa mara moja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Kwa miaka ya karibuni, anakuwa Rais wa kwanza wa kizazi kipya wa Tanzania kutunukiwa Shahada ya Heshima na Chuo kikubwa chenye heshima kubwa duniani cha Jawaharlal Nehru cha India huku akiandika historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kutunukiwa Shahada ya Heshima na Chuo hicho na Rais wa 3 pekee baada ya Rais wa Urusi, Vladimir Putin pamoja ya Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Japan Hayati Shinzo Abe kutunukiwa na Chuo hicho.

Ndani ya miaka mitatu, Rais Samia ameshatunukiwa Shahada 4 za Udaktari wa Heshima pamoja na Tuzo na kutajwa kwa zaidi ya mara 5 kutoka kwa majarida na taasisi mbalimbali kubwa za kimataifa kwa kutambua kazi yake kubwa anayoifanya kusukuma maendeleo kwenye Taifa lake. 

Tayali Jarida maarufu la Avance Media la Ghana lilimtaja kama mmoja wa Wanawake 100 wa Afrika wenye nguvu na ushawishi mkubwa Barani Afrika kabla ya Majarida mengine makubwa yanayosomwa duniani kote kama The Time na Forbes ya Marekani kumtaja pia miongoni mwa Wanawake 100 wenye nguvu ulimwenguni huku Chama Cha Waandishi wa Habari za Miundombinu na Fedha Afrika (MIFA) wakimchagua na kumpa Tuzo pia Rais Samia kama Rais aliyefanya mapinduzi makubwa zaidi ya miundombinu Barani Afrika kwa mwaka 2022.

Haya yote yanafanywa kwa kutambua jitihada zake kubwa za kuendeleza mageuzi ya kijamii, kisiasa na kiuchumi kupitia mtindo wake wa uongozi unaoamini katika 4R kama maridhiano katika kujenga Taifa imara na la pamoja. 

Uamuzi huu ni wa kutambua uongozi wa kipekee wa Rais Samia katika kuendeleza mageuzi ya kijamii, kisiasa na kiuchumi nchini Tanzania. 

Mageuzi hayo yameboresha ustawi wa Watanzania, kukuza sifa ya Tanzania duniani kote na kuendeleza uhusiano wa kibiashara, kiuchumi na kisiasa kati ya Tanzania na nchi nyingine kote duniani na ndiyo mana leo kuanzia Januari 27-28, 2025 Tanzania kunafanyika Mkutano wa Nishati wa Dunia na Viongozi wakuu wa nchi zaidi ya 30 wako Tanzania na ulimwengu mzima kujadili masuala ya nishati. Hii yote ni ushawishi mkubwa wa Rais Samia kwasasa kwenye siasa za ulimwengu.

Nje ya maisha yake toka kuzaliwa, elimu na utumishi, Rais Samia ameolewa na Bwana Hafidh Ameir na wamejaaliwa watoto wanne, watatu wakiwa wakiume na mmoja wa kike.

Huyu ndiye Mwanamke wa Shoka, asiyelaza zege, Muumini wa Vitendo kuliko maneno, mbeba maono na Msikivu kwelikweli ambaye tunasherekea miaka yake 65 iliyotukuka.





*MAKALA HII IMEANDIKWA NA BWANKU M BWANKU AMBAYE NI AFISA TARAFA YA KATERERO ILIYOPO BUKOBA MKOANI KAGERA.*

Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

Wananchi Serengeti Wamtaja Dkt Rhimo Nyansaho Kama Chachu ya Maendeleo Kwao

Na Shomari Binda-GMTV  WANANCHI Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamemtaja Dkt.Rhimo Nyansaho kama chachu ya maendeleo kupitia taasisi yake ya Nyansaho Foundation. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na GMTV wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu mchango wake umeonekana katika kuisaidia jamii. Wamesema ukifika Jimbo la Serengeti kila Kata na Kijiji huwezi kukosa mkono wa Dkt.Nyansaho kuchangia na kusaidia jamii kuanzia elimu,afya,maji na masuala mengine ya jamii. Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mwita Sagati amesema wapo watu wanaojitokeza kusaidia jamii kipindi cha uchaguzi kwa kulenga kupata uongozi lakini imekuwa tofauti kwa Dkt.Nyansaho. Sagati amesema iwapo atajitokeza kuomba nafasi ya ubunge wapo tayari kumpambania na kumchagua ili aweze kuendelea kutoa mchango wake katika kusaidia jamii. " Tunashukuru sana mchango wa Dkt.Nyansaho kwa kuchangia shughuli za maendeleo hapa Serengeti. " Wengine huwa wanakuja nyakati za uchaguzi lakini huyu mchango wake ni ...

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...