CCM Mkoa wa Mara yamtakia Heri ya Kuzaliwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan

GEORGE MARATO TV
0



Na Shomari Binda-Musoma 

CHAMA cha Mapinduzi ( CCM)mkoa wa Mara kinaungana na watanzania kumtakia heri ya kuzaliwa Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan



Salam hizo zimetolewa na Katibu wa CCM mkoa wa Mara Ibrahim Mjanakher alipokuwa akizungumza na GMTV ofisini kwake.

Amesema katika siku ya leo januari 27 inaposherehekewa siku ya kuzaliwa ya Dkt.Samia CCM mkoa wa Mara na wananchi hawana budi kumpongeza kwa mazuri aliyoyafanya kwenye mkoa.

Amesema kwa kipindi kifupi mkoa umepokea zaidi ya tilioni 1 kwaajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo.


Mjanakher amesema ukifika mkoa wa Mara utaona mabadiliko makubwa zikiwemo shule nzuri zilizojengwa,hospitali,miradi ya maji,barabara na mingineyo.

Amesema kutokana na mazuri hayo wana kila sababu ya kumpongeza na kumtakia heri katika siku yake ya kuzaliwa.

" Tunamuombea maisha marefu Mama Samia na kumtakia majukumu mema anapokuwa anawahudumia watanzania hapa nchini.

" Ukifika mkoa wa Mara utayaona mazuri ambayo tumefanyiwa na Rais Dkt.Samia na ndio maana tunasimama kifua mbele kumpongeza"amesema

Amesema UWT Wilaya ya Musoma mjini wana kila sababu ya kuandaa sherehe ya kumpongeza kama walivyofanya na kila mmoja ana sababu ya kufanya hivyo.





Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top