▪️Awapatia miradi ya Kiuchumi na kutunisha mfuko wa Kikundi.
▪️Wafanyabiashara wamshukuru kwa kuwajali na kuwaendeleza kiuchumi
▪️Wampongeza Rais Samia kuboresha miundombinu ya masoko Jijini Dodoma
📍Dodoma
Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini Mh. Anthony Mavunde ameahidi kuwaendeleza kiuchumi wafanyabiashara wa soko la Sabasaba Jijini Dodoma kwa kuwapatia miradi mbalimbali ya kiuchumi ili kuongeza kipato chao.
Mh. Mavunde kayasema hayo leo wakati wa Mkutano wa Kikundi cha Twiga cha wafanyabiashara wadogo wadogo uliofanyika ndani ya Soko la Sabasaba.
“Tunaishukuru serikali chini ya uongozi wa Mh Rais Dkt. Samia S . Hassan kwa maboresho makubwa ya miundombinu yanayoendelea ndani ya Jiji la Dodoma.
Nipo hapa leo kama Mwanachama mwenzenu wa kikundi cha Twiga ambacho tulikiasisi pamoja.
Nina furaha kubwa kusikia mipango iliyopo ya kuongeza miradi ya kujiimarisha kiuchumi,nitajitahidi kuendelea kuwashika mkono ili muweze kusima










