Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Januari 26, 2025 amewasili Mpanda mkoani Katavi ambapo atakuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa CCM jimbo la Katavi unaofanyika katika viwanja vya TARURA.
Kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda amepokelewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Iddi Kimanta,Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwamvua Mrindoko na Mbunge wa jimbo la Katavi Mhandisi Isaack Kamwele.



