Na Angela Sebastian
Naibu waziri wa maji Mhandisi Kundo Mathew amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan amebadilisha changamoto za wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bakoba vijijini mkoani Kagera na kuwa fursa .
Methew amesema fursa hiyo inakuja baada ya Dk.Samia kutoa kiasi cha shilingi bilioni 15.8 kwa ajili ya kutekeleza mradi mkubwa wa maji wa Kemondo-Maruku unaotarajiwa kunufaisha wananchi zaidi ya laki moja wa kata sita ili kuondokana na kero ya upatikanaji wa maji safi na salama.
Methew ametoa kauli hiyo leo baada ya kutembelea na kukagua hatua ya ujenzi iliyofikiwa kwa sasa kisha kuongea na wananchi na watumishi wa wakala wa maji Vijijini (RUWASA) na mamlaka ya maji safi na maji taka (BUWASA) ,katika maeneo ya Kemondo kinapojengwa chanzo cha mradi huo na Kanazi lilipojengwa tanki.
"Rais Dk Samia anapoleta mradi wa maji anabadilisha kero,changamoto na shida za maji kwa wanachi wake hususani nyie wa Bukoba vijijini kuwa fursa ambazo ni kupata ajira,biashara na ongezeko la mapato katika halmashauri zetu, kutokana na ajira au biashara kwani watu watalipa kodi hivyo, changamoto ya maji katika nchi yetu Dk.Samia anaitatua na kuitimisha kwa kubadilisha kuwa fursa kwetu"ameeleza Methew
Amesema zaidi ya shilingi bilioni tisa zimekwishalipwa kwa mkandarasi ndiyo maana inashuhudiwa mradi huo kufika katika hatua hiyo ambapo kuanzia kwenye chanzo (kidakio )mpaka kwenye tanki ni kilomita nne mpaka sasa kilomita 3.7 maji tiyali yamefikishwa huku mita 300 ikiwa katika hatua za mwisho za kukamilika.
"Hapa tulipofikia zaidi ya shilingi bilioni tisa zimekwishalipwa ndiyo maana tunashuhudia mradi huu kufika katika hatua hii ambapo kuanzia kwenye chanzo (kidakio )mpaka kwenye tanki ni kilomita nne mpaka sasa kilomita 3.7 maji tiyali yamefikishwa huku mita 300 ikiwa katika hatua za mwisho kukamilika"amesema Methew
Alisema kuwa changamoto za maji zimefiki ukingoni kutokana na wataalam walioko chini ya Wizara hiyo kufanya kazi usiku na mchana hivyo, muda mfupi ujao maji yataingia kwenye tanki na kazi hiyo nzuri iliyofanywa na Wizara hiyo inakwenda kukamilika kabla ya mwezi Oktoba mwaka.
Pia amesema maelekezo ya Dk.Samia ni kwamba maji hayo yawe na gharama nafuu hivyo hakuna mtu wa kudhubutu kukiuka maagizo hayo kwasababu ni sheria hivyo tunatii shetia bila shuruti.
Amesema wizara hiyo itaendelea kutekeleza maelekezo yanayotolewa na chama cha Mapinduzi (CCM) nankuwa wasikivu wakati wote.
Naye katibu wa CCM wa Wilaya ya Bukoba Vijijini Jesca Ndyamukama amepongeza uongozi wa Dk.Samia na Wizara ya maji kwa kazi kubwa na mipango mikubwa anayoendelea kufanya hususani utekelezaji wa miradi ya maji nchi nzima kuni hari hiyo inaleta matumaini kwa wananchi .
Kaa upande wa diwani wa kata ya Kemondo Hatwibu Mussa amesema mradi huo ulianza mwak 2021 ambapo hapo katika ulianza kusuasua na kusababisha maneno mengi kutoka kwa wananchi hivyo kwaasasa tunayo matumaini na tunamshukuru Rais Dk.Samia Suluhu Hassan mwenyezi Mungu aendelee kumtinza ili athletes maendeleo zaidi.
Mradi huo wa Kemondo- Maruku ambao ulianza utekelezaji wake katika bajeti ya 2021/2022 unaotarajiwa kunufaisha wananchi wapatao laki moja kutoka katika kata sita unaelekea hatu ya mwisho ya utekelezaji ambapo kabla ya mwezi Oktoba mwaka huu utakuwa umekamilika na wananchi kupata maji safi na salama.