Mbunge wa jimbo la Musoma mjini Mhe Vedastus Mathayo leo 08/01/2025 ameshiriki semina iliyoandaliwa kwa ajili ya viongozi wa Serikali za mitaa katika halmashauri ya Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
Semina hiyo ya kwanza tangu viongozi hao wachaguliwe Novemba 27 mwaka 2024 imefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Manispaa ya Musoma.
Akizungumza na viongozi hao wa Serikali za mitaa Mhe Mathayo pamoja na mambo mengine, amekemea vitemdo vya rushwa katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
Semina hiyo imefunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Musoma Mhe Juma Chikoka.