Kupitia *#MORNINGJAM* ya *CAPITAL RADIO,* leo Afisa Uhifadhi Mkuu na Mkuu wa Idara ya Mawasiliano - TANAPA, Catherine Mbena akitoa elimu ya Uhifadhi na Utalii ikiwemo kufuata sheria, taratibu, na miongozo ya watalii wa ndani na nje kufuata wanapokuwa ndani ya Hifadhi za Taifa kwa ustawi wa Uhifadhi na Utalii nchini.
Elimu ya Uhifadhi na Utalii imeendelea kutolewa kupitia vyombo mbalimbali vya Habari nchini na kuwakumbusha wanajamii umuhimu wa kushirikiana na TANAPA katika kulinda maliasili hizo.