Kamati ya Siasa kata ya Bweri Manispaa ya Musoma Mkoani Mara,imemkabidhi hati mbili mbunge wa jimbo la Musoma mjini Mh Vedastus Mathayo kwa kutambua mchango mkubwa wa maendeleo ambao ameufanya katika kata hiyo na jimbo zima la Musoma mjini.
Mbali na kumkabidhi hati hizo kamati hiyo ya siada pia imempongeza mbunge huyo kwa kazi nzuri anazozifanya za kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo la Musoma mjini na kuwa kiongozi msikivu na mpenda watu.
Akikabidhi hati hizo za pongezi, Mwenyekiti wa ccm kata ya Bweri Ndg Munyu Matara,amesema CCM kata ya Bweri inampongeza sana mbunge Mathayo kwa kazi nzuri, nakumuomba aendelee kuchapa kazi na asisikilize maneno ya watu.
Akitoa neno la shukrani, mbunge wa jimbo la Musoma mjini Mhe Vedastus Mathayo, ameishukuru sana kamati ya Siasa kata ya Bweri kwa zawadi ya hati na kutambua mchango wake wa maendeleo kwenye kata hiyo.