Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mwigulu Nchemba: Kutoka kuchunga ng'ombe hadi Uwaziri Mkuu wa Tanzania




Mwigulu Lameck Nchemba Madelu ni Waziri Mkuu mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni mwenyeji wa mkoa wa Singida na kwa sasa ana umri wa miaka 50.


Uteuzi wake umetangazwa rasmi bungeni mjini Dodoma, katikati mwa Tanzania  na baadaye kuthibitishwa na bunge, kwa mujibu wa Katiba ya nchi . Amethibitishwa kwa kura 369 za ndio kati ya 371 zilizopigwa na wabunge mbili zikiharibika.


Mwigulu anajulikana kama mfano wa mafanikio yanayotokana na bidii na kujituma. Alikulia katika mazingira ya kijijini na alitoka katika familia yenye hali ya kawaida, ambapo aliwahi kuchunga ng'ombe nyikani akiwa kijana mdogo. Maisha hayo yalimfundisha nidhamu, uvumilivu na kuthamini kazi halali. Mara kadhaa amekuwa akisimulia hadithi ya maisha yake kama njia ya kuwahamasisha vijana kupambana kupitia elimu na kujituma.


"Mimi umasikini wa Tanzania sijausoma kwenye kitabu nimeuishi, miaka takribani 32 nimeishi katika maisha hayo ya umasikini", alisema Nchemba mara baada ya kuthibitishwa bungeni. "Unaenda kuchunga ukirudi nyumba nzima inavuja, natambua maisha haya". Anasema Nchemba.


Alisoma shule ya msingi Makunda mkoani Singida kati ya mwaka 1987 hadi 1993, kisha akaendelea na masomo ya sekondari katika shule ya sekondari Ilboru mkoani Arusha na sekondari ya Mazengo mkoani Dodoma ngazi ya kidato cha tano na sita. Baada ya hapo alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako alisomea shahada ya kwanza ya uchumi na baadaye akahitimu shahada ya uzamili mwaka 2006, na baadaye kupata shahada ya uzamivu kutoka chuo hicho hicho.


Safari ya kisiasa ya Mwigulu


Safari yake ya kisiasa ilianza kupanda kasi mwaka 2010 aliposhinda ubunge wa Jimbo la Iramba Magharibi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Alirudi tena bungeni mwaka 2015. Ndani ya chama chake amejipatia heshima kama kiongozi mwenye msimamo thabiti na anayejali nidhamu katika utumishi wa umma. Amewahi kuwa Katibu Mkuu Msaidizi, mjumbe wa Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na sekretarieti ya chama kwa miaka mingi.


Dkt. Mwigulu amewahi kushika nafasi mbalimbali serikalini. Alianza kama Naibu Waziri wa Fedha katika serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete. Baadaye aliteuliwa kuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi mwaka 2015, kabla ya kuhamishiwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi mwaka 2016. Mwaka 2021 aliteuliwa kuwa Waziri wa Fedha, nafasi aliyoishikilia hadi uteuzi wake kuwa Waziri Mkuu.


Mwaka 2018 aliondolewa katika nafasi ya Waziri wa Mambo ya Ndani baada ya Rais wa wakati huo, John Magufuli, kueleza kuwepo kwa changamoto katika wizara hiyo ikiwemo matumizi mabaya ya fedha na kasoro katika baadhi ya mikataba ya serikali. Pia alimlaumu kwa kutumia muda mwingi katika mitandao ya kijamii badala ya kufanya kazi za umma ikiwemo kudhibiti ajali za barabarani. Hata hivyo, Mwigulu aliendelea kuwa miongoni mwa wanasiasa wenye ushawishi mkubwa ndani ya chama chake.



Hamia Burundi" kauli tata ya Mwigulu inayoishi


Kauli yake maarufu iliyoibua mjadala mkubwa ilitolewa mwaka 2021 alipokuwa akiwasilisha bajeti akiwa Waziri wa Fedha. Baada ya kuulizwa kuhusu malalamiko ya wananchi juu ya kodi kwenye miamala ya simu, alisisitiza kuwa sheria ikishapitishwa na bunge haina budi kutekelezwa, akiongeza kwa utani kwamba "anayehisi afadhali kuhamia Burundi, basi aende tu." Kauli hiyo ilitawala mijadala kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kwa muda mrefu.


Mwigulu ni mtu anayejulikana kwa uzalendo wake. Mara nyingi huonekana akiwa amevalia skafu yenye rangi za bendera ya taifa, akisisitiza umuhimu wa kuipenda Tanzania. Pia amekuwa akisaidia vijana hasa katika masuala ya elimu, akiamini kuwa elimu ndiyo njia kuu ya kupambana na umasikini.


Uteuzi wake kuwa Waziri Mkuu uliwashangaza watu wengi, kwani jina lake halikuelezwa sana katika mijadala ya awali. Wakati wa uteuzi huo, majina kama ya Dk. Tulia Ackson, Paul Makonda, Profesa Kitila Mkumbo na Dotto Biteko ndiyo yalikuwa yakitajwa zaidi. Hata hivyo, Rais alimteua Mwigulu kutokana na uzoefu wake serikalini na uwezo wake wa kuongoza shughuli za serikali bungeni kwa ufanisi.


Uteuzi wake umeleta hisia mseto



Mmoja wa wabunge wa muda mrefu, William Lukuvi alisifu uteuzi wake.


"Tunajua uvumilivu alionao Mwigulu kwa mema na mishale mingi aliyopigwa lakini hajatetereka" alisema Lukuvi. Huku Mwanasheria Mkuu, akiongeza "Kwa uzoefu wa Mwigulu Nchemba ni mtu sahihi wa nafasi hii ya uwaziri mkuu".


Hata hivyo, wapo wanaona, Nchemba ni sura ilele ile kwenye serikali ile ile, ingawa uteuzi wake haukutarajiwa.


"Uteuzi wake haukutarajiwa na wengi, majina yaliyokuwa yanatajwatajwa halikuwepo kabisa, ila sidhani kama analeta kitu kipya sana, kwa kuwa amekuwa serikali kwa zaidi ya muongo mmoja na kwa nafasi nyeti", alisema mmoja wa wanahabari wa siasa za Tanzania.


Mbunge wa upinzani kutoka ACT- Wazalendo Addo Shaibu mbali na kuunga mkono uteuzi wake. "Ni mtu mchapakazi, kwetu sisi tulio wachache tunakuunga mkono, kama ishara ya kukupesha imani, tukiwa na imani kwamba utachapa kazi. Tunaimani utasimamia vizuri serikali na rasilimali za taifa, na utasimamia maboresho ya upatikanaji wa katiba mpya", alisema Addo.


Baada ya kuthibitishwa na Bunge, Nchemba alisema "Natambua ukubwa wa kazi iliyo mbele yetu, kazi kubwa kwa watanzania wote", alirejea Dira ya Tanzania ya 2050, akisema imewalenga vijana aiongezea kusimamia upatikanaji wa ajira karibu milioni 8.


"Watanzania wote watasikilizwa katika ofisi za umma", ilikuwa kauli iliyoshangiliwa bungeni, akionyesha anakuja kuleta jambo jipya kwenye utendaji wa Serikali. Aliwatahadharisha watumishi wa Serikali, "Nitakuja na fyekeo na rato".


"Bila amani haya yote hayawezi kufikiwa, tumtangulize Mungu" alimaliza hotuba yake ya kwanza bungeni baada ya kuthibitisha Novemba 13, 2025.


Nchemba anakuwa Waziri Mkuu wa 12 wa Tanzania, akifuata nyayo za Mawaziri wengine Wakuu Tanzania, Julius Kambarage Nyerere 1960-1962, Rashidi Kawawa 1962–1962 na tena 1972–1977, Edward Moringe Sokoine 1977-1980 na 1983-1984 na Cleopa David Msuya 1980–1983 na tena 1994-1995.


Wengine ni Salim Ahmed Salim 1984–1985, Joseph Sinde Warioba 1985–1990, John Malecela 1990-1994, Frederick Sumaye 1995-2005, Edward Lowassa 2005-2008, Mizengo Pinda 2008–2015 na Kassim Majaliwa 2015-2025, anayemaliza muda wake sasa.

Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

Wananchi Serengeti Wamtaja Dkt Rhimo Nyansaho Kama Chachu ya Maendeleo Kwao

Na Shomari Binda-GMTV  WANANCHI Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamemtaja Dkt.Rhimo Nyansaho kama chachu ya maendeleo kupitia taasisi yake ya Nyansaho Foundation. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na GMTV wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu mchango wake umeonekana katika kuisaidia jamii. Wamesema ukifika Jimbo la Serengeti kila Kata na Kijiji huwezi kukosa mkono wa Dkt.Nyansaho kuchangia na kusaidia jamii kuanzia elimu,afya,maji na masuala mengine ya jamii. Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mwita Sagati amesema wapo watu wanaojitokeza kusaidia jamii kipindi cha uchaguzi kwa kulenga kupata uongozi lakini imekuwa tofauti kwa Dkt.Nyansaho. Sagati amesema iwapo atajitokeza kuomba nafasi ya ubunge wapo tayari kumpambania na kumchagua ili aweze kuendelea kutoa mchango wake katika kusaidia jamii. " Tunashukuru sana mchango wa Dkt.Nyansaho kwa kuchangia shughuli za maendeleo hapa Serengeti. " Wengine huwa wanakuja nyakati za uchaguzi lakini huyu mchango wake ni ...

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...