Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Msama amesema ujio wa Rais Samia katika jiji la Dar es Salaam ni tukio muhimu linaloonesha dhamira yake ya kukutana na wananchi na kuwasikiliza moja kwa moja kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29. Amefafanua kuwa Rais Samia amekuwa akipokelewa kwa shangwe na hamasa kubwa katika mikoa yote aliyoitembelea, hali inayoonyesha mapenzi makubwa ya wananchi kwake.
“Rais wetu amezunguka katika mikoa mingi na kila alipofika amepokelewa kwa furaha kubwa. Sasa anakuja Dar es Salaam, hivyo ni jukumu letu wakazi wa jiji hili kujitokeza kwa wingi kumpokea na kumuunga mkono katika kampeni zake ambazo zitafanyika katika maeneo ya Kinondoni,












