Mgombea Ubunge wa Itilima Kwa Ccm Ndugu Njalu Ahimiza Amani na Utulivu

GEORGE MARATO TV
0


Mgombea Ubunge jimbo la Itilima kupitia chama Cha Mapinduzi Njalu Daudi Silanga Maarufu Profesa wa Maendeleo  ameendelea na kampeni kijiji kwa kijiji kuomba kura kwa wananchi yeye mwenyewe,Madiwani  na kumuomba kura Mgombea Urais wa CCM Dkt Samia Suluhu Hassan  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 

Njalu amefanya mikutano  ya Kampeni katika vijiji vya Nyantugutu,,Mwamalinze,Gaswa na Mwabuki ,huku mikutano yake ikihudhuriwa na mamia ya wananchi wanaokuja kusikiliza Sera za chama cha mapinduzi kwa ilani ya Ccm ya mwakan2025/2030  ambayo imelenga kuwaletea maendeleo wananchi.

Akinadi Sera kwa  wananchi wa vijiji hivyo  Njalu amesisitiza upendo amani na utulivu siku ya tarehe 29 oktoba huku akiwaomba kujitokeza kwa wingi kupiga kura kumchagua Dkt Samia, kura za  ndiyo kwa Mbunge Njalu Silanga na  Madiwani wa CCM.




"Leo Itilima tunajivunia hapa tulipo kwa sababu ya upendo na ushirikiano wetu ninawaomba ndugu zangu tuilinde amani na umoja huu ili siku ya tarehe 29 oktoba tujitokeze kwa pamoja tukaichague CCM kuanzia kwa Dkt. Samia mama ambaye utendajikazi na upendo wake kwa watanzania Siyo wa kutilia mashaka amesema Njalu 

" lakini pia Ninaomba kura za ndiyo ili kwa pamoja tuendelee kuijenga Itilima yetu na msisahau kupiga kura kwa Madiwani wote wa CCM.











Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top