Maelfu ya Wananchi wa Pemba Wajitokeza Kumsikiliza Dkt Nchimbi

GEORGE MARATO TV
0

 Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi, ameendelea na ziara yake ya kampeni visiwani Zanzibar ambapo leo Oktoba 8, 2025, amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Pemba.

Mara baada ya kuwasili, Dkt. Nchimbi alilakiwa kwa shamrashamra na mamia ya wananchi, viongozi wa chama na jumuiya mbalimbali za CCM waliojitokeza kumpokea kwa hamasa kubwa.









Katika siku ya leo, Dkt. Nchimbi anatarajiwa kuanza mikutano yake ya hadhara katika Mkoa wa Kaskazini Pemba, eneo la Kinyasi – Wete, kabla ya kuelekea Mkoa wa Kusini Unguja, ambako atahitimisha kwa mkutano mkubwa wa kampeni katika Jimbo la Chwaka.

Ziara hiyo ni sehemu ya mwendelezo wa mikutano ya kampeni ya CCM kusaka ushindi wa kishindo kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan (Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania), pamoja na wabunge na madiwani kote nchini.














Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top